News Alert: Mwandishi wa Habari Mwanadada,Elizabeth Mayemba afariki dunia ghafla

TANZIA: 

Mwandishi Mwandamizi wa Habari za michezo na burudani wa gazeti la Majira, Elizabeth Mayemba amefariki dunia usiku wa leo baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake eneo la Tabata kwa Swai jijini Dar es Salaam.

Taaifa za awali zinaeleza kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku huu wa Julai 9.2016,ambapp inaelezwa alikuwa akijisikia kizunguzungu na ndipo alipopatwa na umauti huo licha  ya kukimbizwa Hospitali.

Aidha, Taarifa kutoka kwa mume wa marehemu, Eliza, Bwana Rogers amebainisha kuwa…, alipigiwa simu saa mbili usiku na kuambiwa Eliza alisikia kizunguzungu ghafla na kuanguka chini, alichukuliwa na kupelekwa hospital baada muda mtu aliyempeleka Eliza hospital alimpigia tena na kumpa taarifa za Eliza kufariki. 

Taarifa nyingine zitatolewa baada ya  ndugu wa marehemu kukutaana. 

RIP Elizabeth Mayemba.

Blog hii ya WANGOFIRA inatoa pole kwa ndugu na jamaa wote popote pale walipo. Ni pigo kubwa katika tasnia ya Habari.

IMG-20160709-WA0136Marehemu Elizabeth Mayemba enzi za uhai wake..

IMG_0960Meneja Mkuu wa Kampuni ya Business Times Limited, Aga Mbuguni, akimkabidhi kombe la bandari Chalenji Meneja wa timu ya netiboli ya Business Times, Elizabeth Mayemba (Enzi za Uhai wake)  baada ya timu hiyo kushinda kombe hilo. Jijini Dar es Salaam.
News Alert: Mwandishi wa Habari Mwanadada,Elizabeth Mayemba afariki dunia ghafla News Alert: Mwandishi wa Habari Mwanadada,Elizabeth Mayemba afariki dunia ghafla Reviewed by WANGOFIRA on 20:18:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.