TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA ELIZABETH MAYEMBA

Elizabeth Mayemba


Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba kilichotokea jana jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai

TASWA imestushwa na kuhuzunishwa  sana kutokana  na kifo hiki cha  Elizaberth ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa unahitajika sana.
Waandishi wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka elizaberth kutokana na usheshi,kujituma na  uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa mfano kwa waandishi chipukizi.

TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa habari na kuwatakia moyo wa  subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.

Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Juma Pinto

Mwenyekiti TASWA
TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA ELIZABETH MAYEMBA TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA ELIZABETH MAYEMBA Reviewed by WANGOFIRA on 20:11:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.