ASSUMPTER MSHAMA AANZA KWA KASI YA MAGUFULI

NA Omary Mngindo, Kibaha
MKUU wa wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Assumpter Mshama ameianza kazi yake kwa kasi ya Rais Dkt. John Magufuli ya kuchapakazi papo kwa hapo huku akisema Serikali hiyo imedhamilia kuwatumikia watu wa hali ya chini.

Mkuu huyo amefanya mkutano wa kwanza kwa kukutana na wafanyabiashara wa soko Kuu la Mailimoja ambapo alipokea kero malimbali ikiwemo ya Mwentekiti wa soko hilo Ally Gongi kukaa madarakani kwa miaka minane huku akiwa pia Mwenyekiti wa SACCOS iloyopo sokoni hapo ambapo wafanyabiashara hao wamesema hatua hiyo inachangia kukwamisha maendeleo ya soko.

Katikakutaka kuondokana na hali hiyo, wafanyabiashara hao walimtaja Mkuu huyo awapatie ridhaa ili wafanye uchaguzi papo hapo ili waoate viongozi wataoliongiza soko baada ya Mwenyekiti wao kukaa  adarakani kwa miaka minane pasiookuitisha uchaguzi, ambapo Mkuu huyo alisema jukumu hilo ni lao na kama wataweza kufanya hivyo haba pingamizi katika kusimamia zoizi hilo.

Baada ya kauli hiyo ikafuatia hatua ya kuoendekeza majina ya watu watano kisha kupigiwa kura kwa kunyoosha vidole ambapo Ramadhani Maulid alifanikiwa kushinda kinyang'anyiro hicho hivyo kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa awali Ally Gongi " Mzee wa Shamba".

Baada ya kufanyika kwa zoezi hilo Mkuu huyo alifanya ziara ya kukagua soko ambapo alijionea  wafanyabiashara wa gari ndogo za kubeba mizigo na baadhi ya wafanyabiashara wakufanyia shughuli zao chini ya Transfoma ya Umeme hatua ambayo ni hatari kwa naisha yao.

Alipokuwa anapita katika soko hilo nderemo, vifijo na vigeregere vilidikika kutoka kwa akina mama huku wakisema wanaikubali Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli huku wakiuliza siku zote Mshsma alikuwa wapi, kwa maana ya kuonesha kuridhishwa na kadi yake ya kazi.
"Serikali hiiya awa u yaTano chuni ya Rais wetu Dkt. John Magufuli imedhamilia kuwatumikiawananchi kwa kuwaondolea adha zinazowakabili, hivyo tupatie ili ushirikiano ili tuchapekazi mkiyokuwa mnaihutaji," alimalizia Mshama.

Pichanini matukio tofauti ya ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani Assumoter Mshama akiookuwa anazungumza na wafanyabiashara wa soko Kuu la Mailimija mjini hapa. Nyingine akiwa anazungukia naeneo ya soko hilo.
ASSUMPTER MSHAMA AANZA KWA KASI YA MAGUFULI ASSUMPTER MSHAMA AANZA KWA KASI YA MAGUFULI Reviewed by WANGOFIRA on 21:11:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.