Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ajiuzulu


Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, ametangaza atajiuzulu baada ya kushindwa kuwashawishi raia wengi wa Uingereza, kusalia katika muungano wa Ulaya. Cameron akiwa amejawa na huzuni amesema kuwa atasalia ofisini kwa siku tisini zijayo ndipo angatuke.

Cameron amesema kuwa kauli ya wengi lazima isikilizwe japo hafahamu kwanini Waingereza walifanya uamuzi kama huo wakati taifa hilo lilikuwa lina ufanisi mkubwa sana ndani ya EU.

Raia wa Uingereza wamepiga kura ya kumaliza uanachama wa Uingereza ndani ya EU uliodumu kwa miaka 43. Watu wanaoishi katika miji ya London na Scotland ndio waliopiga kura kwa wingi kusalia ndani ya muungano huo.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahofu athari za kujiondoa kwa Uingereza kwenye muungano huo utabainika katika masoko ya hisa huku kukitarajiwa athari kubwa kiuchumi, kisiasa ndani na nje ya bara la Ulaya.

Kura 17,410,742 zilitaka Uingereza iondoke na kura 16,141,241 walitaka Uingereza isalie

Source BBC.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ajiuzulu Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron ajiuzulu Reviewed by WANGOFIRA on 02:22:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.