UVCCM: Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia mkutano wa CCM.



Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) umesema kuwa hakuna mtu au kundi la watu au taasisi yenye ubavu wala uthubutu wa kuuzuia au kuukwakisha kwa namna yoyote mkutano mkuu wa CCM unaoitarajiwa kufanyika Julai 23 mwaka huu .
Aidha umoja huo umesisisitiza  kwamba mkutano huo utafanyika vile vile  kama ilivyopangwa hivyo kuwataka *Bavicha* waache kupiga kelele hovyo na kutoa vitisho vya kitoto.
Msimamao huo umetangazwa  jana na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM *Shaka Hamdu Shaka* alipozungumza na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM mkoa Iringa katika jengo la CCM akiwa njiani kuelekea Ihemi mkoani hapa.
Shaka alisema UVCCM wako tayari kuidhihirishia dunia kwa kuwatia adabu Bavicha ikiwa siku moja watajaribu  kufanya jambo lolote  linalotishia kuhatarisha usalama au ustawi wa maendeleo ya kisiasa ya CCM kwa saa, siku,  wakati na mahali popote.

Alisema siku moja ikitokea Bavicha kutenda jambo lolote la hujuma au kudhuru, UVCCM haitaomba kibali au ruhusa ya viongozi wa juu wa  CCM  badala kitakachotokea  dhidi yao  ni matokeo mabaya ambayo  yatakayongia katika vitabu vya historia ya kuogofya .
"Tunalaani tishio la kipuuzi la Bavicha , tunataka kuona jeuri yao, ubavu na misuli yao ili  kuuuzuia mkutano  maalum wa CCM Julai 23 mwaka huu, watakavyokuja sivyo watakavyorudi, wajaribu ili wakione kipurepure cha marombe siku  watakapojaribu."alisema Shaka.
Tamko hilo  la Shaka linafuatia kauli iliotolewa hivi karibuni na viongozi wa Bavicha wakitishia kufanya lolote ili kuhakikisha mkutano mkuu maalum wa CCM hautafanyika mkoani Dodoma mwezi  ujao.
Aidha Kaimu huyo Katibu mkuu alisisitiza  ikiwa Bavicha na Chadema wameshindwa kuendesha siasa za kiungwana zinazoheshimu na kufuata misingi ya kikatiba na kisheria , UVCCM haitashindwa kutia ndimi zake puani au kubadili kurasa za historia mwanana iliopo .
Shaka aliwataka Bavicha kuacha siasa za mikwara, vitisho, kutishia usalama na amani ya nchi kwa kuijifanya vijogoo wakati hawana lolote wanaloweza aidha kuzuia,  kujenga au kubomoa .
Shaka alisema Bavicha lingekuwa Baraza makini, lenye vijana wa kisasa wenye maarifa, upeo na upembuzi wa kisiasa lingewakemea wabunge wanaosusia vikao vya bunge.
"Wasingekaa bila ya kuwaasa au kuwaonya wabunge wao wanaoshinda kwenye viwanja vya bunge wakipuuzia dhamana ya kuchaguliwa  au kujua maana na mantiki ya misingi ya  uwakilishi bungeni " alieleza
Alisema kukaa kimya kwa Bavicha bila kuonyesha na kutowaelekeza viongozi wao ni wazi  Baraza hilo limefiisika, halina vijana wenye ujasiri,  maamuzi wala  weledi hivyo ni sawa  na mbwa anayebweka nyakati za usiku  akiwa hana meno ya kuuma .
Hata hivyo Shaka aliwataka makatibu wote wa makao makuu UVCCM na wilaya kuendelea na maandalizi ya kuwanoa kiitifaki  *Green Guard* ambao watakuwa  macho kwa kazi malum za kulinda mali za chama na usalama wa viongozi toka sasa hadi kumalizika kwa mkutano maalum Julai 23 mwaka huu .
Hapa ndipo utakapoona tafauti ya CCM na Vyama vingine.
"sisi ni chama cha Siasa wenzetu wana mashirika ya kisiasa lazima tuwaoneshe wananchi utofauti wetu  endeleeni kujiandaa vizuri kimkakati ili tufanikishe mkutano mkuu wetu kwa mafanikio makubwa ili tuzidi kuidhihirishia dunia kuwa CCM ni chuo cha democrasia hakuna mwenye ubavu wa kuzuwia mkutano mkuu maalum Dodoma."
Huku akiongeza;  "kama yuko anaetaka kuijaribu UVCCM tunamwambia ajaribu aone ifike pahala kuwe na kikomo paka hachewi sharubu kirahisi rahisi."
alionya shaka Hamdu.
UVCCM: Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia mkutano wa CCM. UVCCM: Hakuna mwenye ubavu wa kuzuia mkutano wa  CCM. Reviewed by WANGOFIRA on 07:13:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.