MADUDU YAIBULIWA HESLB


WAZIRI wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ametangaza kiama kwa watendaji wote wa Bodi ya Mikopo waliofanya ubadhirifu wa fedha za wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa kuwapa watu wasiohusika.


Joyce ameyasema leo wakati akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa bodi ya mikopo baada ya kufanya ukaguzi maalum katika hoja 17 ni hoja moja imepata majibu na kuzaliwa dosari zingine ambazo ni kutokuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu kwa watu ambao wanarejesha mikopo.

Amesema kuwa kutokana na matatizo ya bodi ya mikopo ameigiza bodi kuhakikisha wanachukua hatua kwa watendaji wote waliosimamishwa ikiwemo kuwafikisha vyombo vya dola.

Joyce amesema kuwa katika dosari nyingine wanafunzi zaidi ya 2,000 wamepewa mikopo katika vyuo viwili lakini wanafunzi hao hawapo katika vyuo vilivyotajwa.

Amesema kuwa kuna wanafunzi wanalipwa sehemu mbili ya mikopo ya bodi kwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa wakati mmoja huku kuna wanafunzi hawapati mikopo kabisa na ni watoto wa masikini.

Aidha amesema bodi hiyo inatakiwa kufanyia kazi dosari zote pamoja na hatua ambazo wamezichukua kwa baadhi ya watendaji ambao wamefuja fedha za walipa kodi.

Joyce amesema kuwa matatizo mengine ni Baraza la Usajili wa vyuo vya Elimu na ufundi (NACTE) kufanya kazi ambazo wao wenyewe hawana uwezo nazo ikiwemo kukagua baadhi ya vyuo ambavyo vingine vinatoa digrii ya pili.

Amesema yote wanaangalia kwa kupitia sheria na kuona jinsi ya kuboresha utendaji kazi kwa NACTE
MADUDU YAIBULIWA HESLB MADUDU YAIBULIWA HESLB Reviewed by WANGOFIRA on 20:09:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.