Basi la Kampuni ya Tahmeed Lilivyoteketea Kwa Moto Barabara ya Chalinze- Segera


Basi la Abiria la Kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga- Dar es Salaam, limeteketea kwa moto katika barabara ya Chalinze- Segera.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiri ndiyo imeteteketea ndani ya basi hilo.

Ajali imetokea wakati basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba Msaada akajisaidie (kuchimba dawa) na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya gari na muda mfupi gari lote likashika moto.



Basi la Kampuni ya Tahmeed Lilivyoteketea Kwa Moto Barabara ya Chalinze- Segera Basi la Kampuni ya Tahmeed Lilivyoteketea Kwa Moto Barabara ya Chalinze- Segera Reviewed by WANGOFIRA on 20:16:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.