Kijana Awafungia Ndugu zake Ndani na Kisha Kuchoma Moto Nyumba

Nyumba moja iliyopo mtaa wa Kiseke Wilayani Ilemela Mkoani Mwanza imeteketea kwa moto leo asubuhi na kuunguza vitu vingi huku wakazi wa nyumba hiyo wakinusurika kupoteza maisha. 


Taarifa zinaarifu kuwa, nyumba hiyo imewaka moto baada ya mmoja wa watoto wa familia hiyo kuamka asubuhi na kumwaga mafuta ya taa katika moja ya chumba cha nyumba hiyo na kisha kuwasha moto 


Imeelezwa kuwa, kijana huyo ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili amekuwa akiwatishia kwa muda mrefu kuwachoma moto lakini wamekuwa wakimpuuza kutokana na matatizo yake ya akili



Baada ya kumwaga mafuta na kuwasha moto, kijana huyo alitoweka na kuwafungia ndugu wengine ndani ambapo majirani walifanikiwa kuwahi kuwaokoa 
 

Je,

Kijana Awafungia Ndugu zake Ndani na Kisha Kuchoma Moto Nyumba Kijana Awafungia Ndugu zake Ndani na Kisha Kuchoma Moto Nyumba Reviewed by WANGOFIRA on 08:16:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.