MUME AMCHINJA MKE NA YEYE KUJINYONGA.


Watu watatu wamefanya mauaji ya kutisha, wawili wamechinja wake zao, huku mmoja akiacha ujumbe wa kumtaka mama yake mzazi amtunzuie watoto na mwingine amemuua mama yake. 

Katika tukio la Dodoma, Samson Joramu(44), mkazi wa Chololo, Kata ya Kikombo, alimchinja mke wake, Rehema Joram (43) kabla ya kujiua kwa kunyonga katika shamba lake.

Watu walioshuhudia walisema, Joramu baada ya kumuua mkewe alijinyonga na aliandika ujumbe uliokutwa mfukoni kwake, ukisomeka: “Mama tunza wanangu, mimi nimekufa.” Kadhalika aliandika orodha ya watu anaowadai. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa akizungumzia tukio hilo alisema kuwa: “Ni kweli taarifa za vifo kutoka Kikombo ninazo, yule mmoja alimuua mama yake kwa kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili jana (juzi), na huyu mwingine alimuua mke wake asubuhi ya leo (jana) kisha naye akajinyonga,” alisema. 

Katika tukio jingine, Amos Kalenda, mkazi wa Kikombo, Dodoma anadaiwa kumuua mama yake mzazi, Joyce Kalenda kwa kumchinja. Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni mama huyo kumnyima chakula. 

Mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime, Wambura Mariba (50) mkazi wa Matongo, Nyamongo, Tarime, anadaiwa kumuua kwa kumchinja mkewe, Maria Wambura(40) kwa madai anamroga. 

Kamanda wa Polisi Tarime/Rorya, Andrew Satta alisema tukio hilo lilitokea Juni 8 saa tisa alasiri. 

Satta alisema baada ya mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo, alichoma moto nyumba zao mbili, zilizokuwa zimeezekwa kwa nyasi. “Baada ya tukio hilo kutokea, wananchi walijichukulia sheria mkononi na kumjeruhi mtuhumiwa kichwani na kitu chenye ncha kali,”alisema Satta. 

Wakizungumzia tukio hilo ndugu wa marehemu, Samwel Wambura alisema tukio la mwanamke huyo kuuawa, lilitekelezwa mbele ya watoto wake wakati akiwaandalia chakula. 

“Alipomaliza kumuua, alianza kuandaa moto achome nyumba ili mwili wa mkewe uungulie ndani, majirani waliwahi kuuchukua mwili, lakini alianza kuwafukuza huku akiwa ameshika panga,” alisema na kuongeza: “Wananchi baada ya kuona tukio hilo walipiga simu kituo cha polisi ambao walifika na kumkamata mtuhumiwa.” 

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto, Kagumiwa Kaijage alisema, alipokea mwili wa marehemu ukiwa umekatwa shingoni na mtuhumiwa amelazwa hospitali hapo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali mwilini.
MUME AMCHINJA MKE NA YEYE KUJINYONGA. MUME AMCHINJA MKE NA YEYE KUJINYONGA. Reviewed by WANGOFIRA on 08:20:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.