Daktari Kortini Akituhumiwa Kusababisha kifo cha Mtoto


Daktari Msaidizi wa Zahanati ya Rwamchanga, Miriam Martine amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kujibu mashtaka ya kusababisha kifo cha mtoto mchanga na kushindwa kumzalisha mama yake.

Akimsomea mashtaka juzi mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Emmanuel Ngaile, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Paschael Nkenyenge alidai kuwa Mei 15, katika zahanati hiyo, mshtakiwa huyo alishindwa kumzalisha mama huyo, Mugesi Juma kwa uzembe na kusababisha mtoto huyo ambaye ni pacha kufa.

Mshtakiwa huyo alikana shtaka na kupatiwa dhamana ya Sh5 milioni za maneno baada ya wadhamini wawili kukidhi masharti yaliyowekwa na mahakama hiyo, ikiwamo mmoja kuwa mtumishi wa umma. Kesi hiyo namba 85/2016, iliahirishwa hadi Mei 27, itakapotajwa tena.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Naomi Nnko alimsimamisha kazi daktari huyo siku moja baada ya kutokea kwa tukio hilo.

Wakati huohuo; Mwalimu wa kujitolea wa Shule ya Sekondari Nagusi wilayani Serengeti, Fikiri Bunduki Mochemba (22) mkazi wa Kijiji cha Singisi amefikishwa mahakamani hapo kujibu shtaka la kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili (17) shuleni hapo.

Mshtakiwa alikana shtaka na kurudishwa rumande hadi Juni mosi.
Daktari Kortini Akituhumiwa Kusababisha kifo cha Mtoto Daktari Kortini Akituhumiwa Kusababisha kifo cha Mtoto Reviewed by WANGOFIRA on 20:50:00 Rating: 5
Powered by Blogger.