DC MAKONDA ATOA WIKI MBILI UKARABATI BARABARA KINONDONI.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda akizungumza na waandishi wa Habari.(picha na Mtapa Wilson.)

Na,  Mtapa Wilson,

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Paul Makonda amewapa wiki mbili watendaji wa halmashauri ya Kinondoni kuanza na kumaliza ukarabati wa mashimo yaliyopo katika barabara zilizoko wilaya ya Kinondoni.

Makonda ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea barabara ya Mwananyamala hospitali, Makumbusho Stand mpaka Akachube ambapo amewataka watendaji wa halmashauri kulekebisha maeneo ya barabara ambayo yameharibika vibaya kutokana na mvua.


AW1A7823
                                      picha kwa hisani ya Milard Ayo blog

“Halmashauri yetu ina magari ambayo yanweza kubeba vifusi ambavyo vinaweza kuwekwa katika mashimo yaliyojitokeza katika barabara zetu kutokana na mvua.  Hii itasaidia angalau kurahisiha barabara zetu kupitika wakati serikali kupitia halmashauri ya Kinondoni ikijipanga kuziboresha zaidi.” Alisema Makonda.


Aidha Makonda alipata fursa ya kuongea na madereva daladala ili kuona zoezi la kubeba walimu bure linavyoendelea ambapo wamemhakikishia kuendelea nalo vizuri kama alivyoagiza..



DC MAKONDA ATOA WIKI MBILI UKARABATI BARABARA KINONDONI. DC MAKONDA ATOA WIKI MBILI UKARABATI BARABARA KINONDONI. Reviewed by WANGOFIRA on 08:58:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.