BAADHI YA SIMU KUTOSAPOTI WHATSAPP IFIKAPO DISEMBA 2016

WhatsApp

Image copyrightGetty
Image captionWakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp, simu nyingi za smartphone zilikuwa za Blackberry na Nokia
Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone 7.1.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”
WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia Desemba 2016.
Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry, WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.
Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.
WhatsAppImage copyrightGetty
Image captionWhatsApp hutumiwa na watu bilioni moja duniani
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa:
  • Android 2.1 and Android 2.2
  • Blackberry OS 7 and earlier
  • Blackberry 10
  • Nokia S40
  • Nokia Symbian S60
  • Windows Phone 7.1
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009, asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia."
WhatsAppImage copyrightReuters
Image captionSimu ya Blackberry
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
BAADHI YA SIMU KUTOSAPOTI WHATSAPP IFIKAPO DISEMBA 2016 BAADHI YA SIMU KUTOSAPOTI WHATSAPP IFIKAPO DISEMBA 2016 Reviewed by WANGOFIRA on 01:25:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.