CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA ELIMU YA JUU (THTU) CHATOA MSAADA HOSPITALI YA SINZA PALESTINA.Kaimu mganga mkuu Hospitali ya Sinza Palestina,Dr. Kayola (kushoto) akipokea msaada kutoka kwa Mwenyekiti wa THTU Bwana Salifius G. Mligo( mwenye koti). picha na Perus Benson

Na, Mtapa Wilson

Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU) tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani wametoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Sinza Palestina kitengo cha wodi ya wazazi wenye gharama ya shilingi 2.5 kama sehemu ya kuzingatia umuhimu na mchango wa mwanawake katika taifa na kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada huo.  Mwenyekiti tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tawi la Mlimani, bwana Salifius G. Mligo amesema kuwa kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba wahudumu wa sekta ya afya nchini na wanawake wakati wa kujifungua, THTU imeamua kutoa msaada huo ili kupunguza matatizo hayo

“Tumeziona juhudi za Viongozi wa Mikoa na Wilaya katika kuunga juhudi za Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za afya katika vituo vya afya, zahanati na hospitali.  Na sisi kama THTU tumefanya haya kama sehemu ya kuunga juhudi hizo”

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu hospitali ya Sinza Palestina, Dk. Crispin Kayola amewashukuru THTU kwa msaada walioutoa kwani imesaidia kuongeza baadhi ya vifaa ambavyo hupungua kulingana na idadi kubwa ya kina mama wanaojifungua hospitalini hapo.

“Kwa wastani hospitali ya Sinza Palestina huzalisha mpaka kina mama 40.  Msaada huu walioutoa THTU utasaidia angalau upungufu wa vifaa vya kujifungulia uliokuwepo awali kama vile mipira (gloves)” Alisema Dk. Kayola.

Nae Elina Sisian, ambae ni mzazi ameziomba taasisi na mashirika mbalimbali kutoa msaada katika vituo vya afya kwani bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili kina mama wakati wa kujifungua katika vituo vya afya.


“bado tunakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vitanda na wodi kwa ajili ya kujifungulia.  Tunaomba taasisi, mashirika na serikali kwa ujumla wasaidie katika hilo.” Alisema  Elina.
CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA ELIMU YA JUU (THTU) CHATOA MSAADA HOSPITALI YA SINZA PALESTINA. CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA ELIMU YA JUU (THTU) CHATOA MSAADA HOSPITALI YA SINZA PALESTINA. Reviewed by Unknown on 08:27:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.