MRISHO MPOTO ANATAFUTA WASANII WATATU WENYE VIPAJI




Msanii wa muziki wa asili na mtunzi wa mashairi, Mrisho Mpoto ameanzisha kijiji kiitwacho ‘Kutoka Shambani’ ambacho kitawakutanisha vijana wenye fani mbalimbali hapa nchini.

11849934_1638965036390349_1427117096_n
Mpoto ameiambia Bongo5 kuwa vijana wenye vipaji mbalimbali na watakaokubali kushiriki watalazimika kukaa miaka 2 kwenye kijiji hicho bila kutumia simu.
“Nilichokifanya nimetafuta heka 20 ambazo zipo, nachofanya nataka nichukue wasani 20 au 30 kutoka kwenye fani mbalimbali, wao watahamia kwenye kile kijiji lakini kwenye muziki nataka kufanya audition kutafuta wasanii watatu, wa kike mmoja, na wa kiume wawili ambao hao wataishi kwenye kile kijiji ambacho tunakiita Kutoka Shambani,” amesema Mpoto.
“Kazi yao kubwa watakuwa wanafuga lakini wanafanya muziki. Nimepata marafiki kutoka mataifa mbalimbali Uingereza na Scotland watakuja kuwafundisha muziki. Pia nitatafuta wataalam wa muziki kutoka hapa ndani pamoja na wasanii wakubwa kama akina Diamond, Alikiba pamoja na Ommy Dimpoz waende wakawatie moyo, wakawatengenezee inspiration,” ameongeza.
“Nataka kuwatengenezea spirit, unajua kinachokosekana hapa ni spirit, na mimi naamini spirit inapatikana katika utulivu, Ndio maana vijana ninaowahitaji ni wale watakaoweza kukaa ndani ya kijiji kwa miaka 2 bila ya simu, yaani simu katika maisha yake ni mwiko. Kwahiyo kwenye wale vijana watatu watakuwa hawana simu wao ni kuimba kufanya show mjini pamoja na kuuza bidhaa zao wanazozalisha kutoka kijijini. Lakini watafanya muziki ambao una asili ya kitanzania,” amesisitiza.
Mpoto amedai anataka kutumia mradi huo kuleta mabadiliko.
“Kuna vitu vingi nimeviangalia na mimi nimekaa kwenye kwenye hili game kwa miaka kama 20 hivi. Lakini sasa hivi Mpoto ameshakuwa legend, natakiwa kuanzisha vitu ambavyo vitaleta mapinduzi pamoja na kutengeneza zao lingile la kizazi kipya. Yaani Mpoto anatakiwa azalishe watu wapya vyenye lengo na mtazamo wa Tanzania na Afrika. Sasa hivi sitaki kufikiria Mpoto anatarekodi lini? Au anatoa nyimbo mpya lini! Nafikiria Mpoto atazalisha watu wangapi na watafika umbali gani! Lakini kwa kuanza nimeona muziki wetu unakutana na changamoto mbalimbali, yaani unabebwa na mazingira ya mataifa mengine. Kwahiyo mimi nilichofanya nikasema nianzishe kijiji Kutoka Shambani.”
“Vijana wote wanaoingia kijijini watalima, wafanya shughuli za uzalishaji, pamoja na Mpoto Foundation ambayo nimeinzisha itakuwa inasimamia na nimeshafika mbali. Nimeshapata support kubwa ya wadau wakubwa, ambao wananisaidia mpaka sasa hivi. Nina support ya Bakhresa yeye ameaiadi chakula cha miaka miwili. Pia Max Malipo wao wamesema wanaweza wakanisaidia milioni 50. Kuna makampuni yamesemwa yasitajwe majina yao, wao wamesema watachimba visima, watafunga solar, wengine wataleta walimu kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.Kuna kampuni wamesema watajenga majumba ya kijiji.
“Kwahiyo itakuwa ni sehemu ambayo watanzania wakitaka burudani wanakwenda na familia zao kupata burudani, kutakuwa na burudani za mchana na za jioni, acha wale wasanii watatu, kuna vikundi vitakuwa vinatoa burudani. Kwahiyo hata watanzania wakati wa weekend watakuwa wanakuja kijijini kupata burudani mbalimbali za muziki wa asili, kupumzika pamoja na kubeba vyakula vya asili ambavyo tunazalisha wenyewe.”
MRISHO MPOTO ANATAFUTA WASANII WATATU WENYE VIPAJI MRISHO MPOTO ANATAFUTA WASANII  WATATU WENYE VIPAJI Reviewed by WANGOFIRA on 06:59:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.