Muhubiri ashtakiwa kwa kusababisha kifo


Pastor Ng'ang'a
Muhubiri mwenye utata James Ng'ang'a ameshtakiwa kwa kusababisha kifo kupitia uendeshaji wa gari vibaya.
Muhubiri huyo aliyewahi kuhudumu kama mhalifu kabla ya kubadilika, alikana mashtaka hayo wakati alipowasilishwa katika mahakama ya Limuru takriban kilomita 200 magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi.
Bwana Ng'ang'a alipelekwa mahakamani chini ya usalama mkubwa kufuatia kukamatwa kwake hapo jana.
Muhubiri huyo atasalia chini ya mikono ya polisi hadi pale kesi yake ya kutaka kuachiliwa kwa dhamana itakaposikizwa na kuamualiwa siku ya ijumaa.
Pia alikana mashtaka mengine matatu ,ya kutoa habari za uongo kwa polisi,kufanya njama za kutaka kukwepa haki pamoja na kushindwa kuripoti ajali.
Wengine walioshtakiwa pamoja na muhubiri huyo ni maafisa wawili wa polisi,mmoja akituhumiwa kwa kujaribu kumsaidia kuficha ajali hiyo ambayo ilimuua mwanamke ,Mercy Njeri mwezi uliopita huku mwengine akituhumiwa kwa kujifanya kama mlinzi wake.
Muhubiri ashtakiwa kwa kusababisha kifo Muhubiri ashtakiwa kwa kusababisha kifo Reviewed by Unknown on 07:03:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.