Rais Nkurunziza aapishwa kwa muhula wa 3


Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza anaapishwa kwa muhula wa tatu uliozua utata.
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge nchini Burundi anasema kuwa sherehe hiyo imefanyika kwa mshangao mkubwa kwa kuwa rais Nkurunziza alitarajiwa kuapishwa wiki ijayo.
Hatahivyo hakuna kiongozi wa taifa lolote aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwake huku Afrika kusini ikishirikishwa na waziri mmoja kulingana na shirika AFP.
Mataifa kadhaa yakiwemo yale ya China na Urusi yalituma mabalozi wao.
Nkurunziza
Mabalozi wa Marekani na muungano wa Ulaya walisusia lakini wakashirikishwa na maafisa wa nyadhfa za chini.
Umoja wa Afrika haukutuma waangalizi.
Takriban watu 10 wameuawa tangu Nkurunziza atangaze mnamo mwezi Aprili kwamba atawania muhula wa tatu wa urais.
Serikali inaushtumu upinzani ambao unasema kuwa muhula huo ni kinyume na sheria kwa kuzua ghasia.
Nkurunziza
Umoja wa Afrika,muungano wa Ulaya na wizara ya maswala ya kigeni ya Marekani wote wameonyesha wasiwasi wao kwamba uchaguzi huo wa mwezi Julai haukuwa huru na wa haki.
Rais Nkurunziza aapishwa kwa muhula wa 3 Rais Nkurunziza aapishwa kwa muhula wa 3 Reviewed by WANGOFIRA on 07:00:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.