Wakonta Kapunda, binti aliyeandika kwa ulimi, apata kifaa

 

  •      Wakonta Kapunda
Unamkumbuka Wakonta Kapunda? Binti Mtanzania mwandishi wa miswada ya filamu anayeandika kwa kutumia ulimi wake?
Wakonta alipata ajali siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita. Ajali hiyo ilimuacha akiwa amepooza kwanzia shingoni kushuka chini na kumfanya kutoweza kutumia mkono yake kuandika.
Wakonta Kapunda
Wiki kadhaa zilizopita, BBC iliporusha habari yake Msamaria Mwema mmoja aliguswa kumsaidia
Kupitia kipindi cha televisheni cha Focus on Africa katika BBC World Service, mwanadada Olivia Soko kutoka Afrika ya Kusini aliguswa kufanya kitu kumsaidia Wakonta.
Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi
Akiwa mkurugenzi wa kampuni ya Whirlmarket Technologies, Olivia alijitolea kutoa msaada wa programu ya kompyuta iitwayo Nuance Dragon Naturally Speaking.
Jinsi Program hii inavyofanya kazi ni kwamba mtumiaji yeye anazungumza anachotaka kukiandika kupitia kipaza sauti chake halafu programu hii inaandika yenyewe katika kompyuta ya mtumiaji
Wakonta alijaribu kuitumia jana, akaifurahia, lakini bila shaka atahitaji muda zaidi ili aizoee vizuri.
Familia yake pia imefurahishwa sana na msaada huu.
Wakonta Kapunda, binti aliyeandika kwa ulimi, apata kifaa Wakonta Kapunda, binti aliyeandika kwa ulimi, apata kifaa Reviewed by WANGOFIRA on 11:14:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.