TAASISI YA MKAPA YA KABIDHI NYUMBA 22 KWA MKOA WA PWANI

Sehemu ya juu ni nyumba hiyo kwa nje kabla haijakabodhiwa na picha ndogo ya chini ni Mgeni rasmi Dkt Kikwete na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wakiwa na madaktari wakiangalia nyumba yenyewe.

Rais Mstaafu  Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mkapa , Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chalinze, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarest Ndikilo , na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wakishiriki kukata utepe kuashiria kukabidhiwa rasmi nyumba hizo,kutoka Taasisi ya Mkapa kwa ajili ya madaktari. 
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa Dr.Ellen Senkoro akimuongoza mgeni Rasmi Dkt Kikwete kwenda kufungua Nyumba hiyo
Baadhi ya wananchi wa Chalinze wakishuhudia ufunguzi wa nyumba hizo za kuishi madaktari katika eneo lao.

Jana Tarehe 13 September 2016 Taasisi ya Benjamin Mkapa ilikabidhi nyumba 22 ilizojenga Mkoa wa Pwani kwa msaada wa Taasisi ya Dunia ya afya ya Marekani. Mradi huo ambao kila nyumba iligharibu Milioni 54  ulikabidhiwa jana kwenye sherehe fupi iliyofanyika Katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze katika kijiji cha Msoga ambapo mgeni rasmi alikuwa Raisi mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete.

Wilaya zilizofaidika na mradi huo ni  Mafia ambayo imepata nyumba 10 , Chalinze 10 na Bagamoyo 2.
TAASISI YA MKAPA YA KABIDHI NYUMBA 22 KWA MKOA WA PWANI TAASISI YA MKAPA YA KABIDHI NYUMBA 22 KWA MKOA WA PWANI Reviewed by WANGOFIRA on 20:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.