Angalia Picha : MOTO MKUBWA WATEKETEZA VIWANDA VYA MBAO MJINI KAHAMA

Eneo la viwanda vya mbao linalojulikana kama eneo la wafanyabiashara wa mbao mtaa wa Majengo katika eneo la stendi ya mabasi madogo mjini Kahama mkoani Shinyanga limeteketea kwa moto.


Inaelezwa kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye mashine ya kukoboa mahindi na kusaga unga wa sembe.

Kwa mujibu wa waandishi wa Malunde1 blog,Shija Felician na Paul Kayanda walioko eneo la tukio wanasema moto huo umeanza kuteketeza mbao majira ya saa 12 na nusu Septemba 14,2016.

Moto huo umebabisha hasara kubwa kwani mbao zote zote zilizopo katika eneo hilo zimeungua moto.

Mbali na mbao kuungua pia mashine zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara wa mbao,watengenezaji wa bidhaa zitokanazo na mbao,milango na vitu vingine vimeungua. 

Juhudi za kuokoa mali katika eneo hilo ziligonga mwamba baada ya gari la jeshi la zimamoto na uokoaji kuishiwa maji,ndipo likaja gari la zimamoto kutoka mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Buzwagi na kusaidia kuzima moto huo.


Kikosi cha zimamoto kutoka mgodi wa Buzwagi kimekuwa msaada mkubwa katika uzimaji wa moto ulioteketeza viwanda vya mbao mjini Kahama na bila msaada kutoka mgodi huo ungeendelea kuteketeza mali za wakazi wa Kahama.

Pia ungeingia kwenye makazi ya wananchi wanaoishi jirani na viwanda hivyo kikiwamo kituo kidogo cha Polisi stendi ndogo Majengo huenda nacho kingeteketea kwa moto huo.
Tutawaletea taarifa kamili baadae.... 
Gari la zimamoto kutoka Mgodi wa Buzwagi likiwa eneo la tukio

Gari la zimamoto likiendelea kuzima moto

Mbao zikiteketea kwa moto

Moto ukiendelea kuwaka


Moto ukiendelea kuwaka

Mfanyabiashara akiokoa mbao zake


Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu akiwa eneo la tukio

Mbao zikiwa eneo la tukio

Gari la zimamoto likiendelea kuzima moto huo

Moto ukiendelea kuwaka
Moto ukiendelea kuwaka-Picha zote na Shija Felician na Paul Kayanda-Malunde1 blog
Angalia Picha : MOTO MKUBWA WATEKETEZA VIWANDA VYA MBAO MJINI KAHAMA Angalia Picha : MOTO MKUBWA WATEKETEZA VIWANDA VYA MBAO MJINI KAHAMA Reviewed by WANGOFIRA on 20:56:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.