NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UENDELEZAJI MILKI
Naibu
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina
Mabula akifungua mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki uliofanyika
kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini Dar es salaam
kwa lengo la kuanzisha Chama chao kwa ajili ya kusimamia masula
mbalimbali ya Uendelezaji wa Miliki , Moja ya mambo yaliyojadiliwa
katika mkuta no huo ni Katiba Pendekezwa ya Chama hicho ambapo wajumbe
wamepata muda wa kuchangia mawazo yao na kurekebisha baadhi ya vifungu
ili kuipitisha mara baada ya kukamilika kwa marekebisho hayo Mkutano huo
umeandaliwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angelina Mabula akizungumzia masuala mbalimbali katika mkutano wa Wadau wa Uendelezaji Milki
uliofanyika kwenye makao makuu ya Shirika la Nyumba NHC Upanga jijini
Dar es salaam
Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Nehemia Mchechu awali
akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dk
Angelina Mabula ili akifungua mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu na Miliki Hamad Abdallah
Mkurugenzi wa wakifuatilia kwa karibu wakati mkutano huo ukiendelea
Baadhi
ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo wakifuatilia kwa karibu
masuala kadhaa ambayo yamezungumziwa katika mkutano huo.
Mmoja wa wadau walioshiriki kwenye mkutano huo Bw. Emilian Rwejuna akiwa pamoja na wadau wengine.
Mkurugenzi
wa Milki Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Hamad Abdallah akifuatilia
maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwanasheria wa Shirika hilo Elias Mwashiuya hayupo pichani wakati akitoa mada kuhusu katiba ya chama hicho katika mkutano huo
Itandula
Gambalagi Mkuu wa Mauzo NHC akisalimiana na Bw. Adam Jee ambaye pia
alihudhuria katika mkutano huo kama mmoja wa wadau wa Uendelezaji Milki.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angelina Mabula na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia
Mchechu wakifuatilia maelezo ya Mwanasheria wa NHC Bw.Elias Mwashiuya
wakati alipokuwa akielezea vifungu mbalimbali kuhusu katiba ya chama
hicho.
Mwanasheria
wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC akitoa maelezo kwa wadau wa
Uendelezaji Milki kuhusu Katiba ya Chama hicho ambayo wadau wamepata
fursa ya kuchangia mawazo yao kabla ya kupitishwa na chama hicho
Wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo
Kutoka
kulia ni Meneja Masoko wa NHC Bw. Tuntufye Mwambusi, Hamad Abdallah
Mkurugenzi wa Milki NHC, Suzan Omari Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NHC
na Mkuu wa Mauzo NHC Bw. Itandula Gambalagi wakiwa katika mkutano huo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM).
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UENDELEZAJI MILKI
Reviewed by WANGOFIRA
on
08:37:00
Rating:
No comments: