Hizi Ndizo Nyimbo 10 Bora Zaidi Kwa Harusi Duniani

Ed Sheeran, 25, akiwa na mashabiki

Wimbo wa mapenzi wa mwanamuziki wa Uingereza Ed Sheeran unaongoza kwa kupendwa sana na watu kama wimbo wa kufungua jukwaa wakati wa harusi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Spotify, ambao wamechunguza maelfu ya orodha ya nyimbo zinazosambazwa zaidi katika mtandao huo, wimbo wa Thinking Out Loud unaongoza.

Wimbo wa At Last wake Etta James ni wa pili nao wimbo wa Ray LaMontagne, You Are the Best Thing ni wa tatu.

Nyimbo nyingine maarufu zilizo kwenye orodha ya 50 bora duniani ni wimbo wake Frank Sinatra uitwao The Way You Look Tonight na wimbo wa Marry You wake Bruno Mars.



Jina halisi la Sheeran ni Edward Christopher "Ed" Sheeran

Nyimbo kumi zinazopendwa zaidi duniani kwa mujibu wa Spotify, mtandao unaowawezesha watu kusikiliza nyimbo moja kwa moja mtandaoni, ni:
Thinking Out Loud - Ed Sheeran
At Last - Etta James
You Are the Best Thing - Ray LaMontagne
All of Me - John Legend
A Thousand Years - Christina Perri
Make You Feel My Love - Adele
I Won’t Give Up - Jason Mraz
Everything - Michael Bublé
Better Together - Jack Johnson
Amazed - Lonestar
Hizi Ndizo Nyimbo 10 Bora Zaidi Kwa Harusi Duniani Hizi Ndizo Nyimbo 10 Bora Zaidi Kwa Harusi Duniani Reviewed by WANGOFIRA on 01:50:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.