Papa: Kuwatumikisha watoto ni utumwa mamboleo

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema kuwa kitendo cha kuwatumikisha watoto kama vibarua ni utumwa mamboleo.
Papa Francis ameitaka jamii ya kimataifa kutokomeza vanzo vya utumikishaji watoto kama vibarua katika maeneo mbalimbali duniani na kukitaja kitendo hicho kuwa ni utumwa mamboleo. Amesema jitihada kubwa zinapaswa kufanywa ili kutokomeza suala hilo.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ameongeza kuwa walimwengu wanapasa kufanya juhudi kubwa ili kutokomeza utumwa huo. Papa Francis amesema kuwa mamilioni ya watoto katika pembe mbalimbali duniani wanakosa haki zao za kimsingi na wanakabiliwa na hatari kubwa.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa hivi sasa watoto karibu milioni 168 wanafanya kazi katika maeneo mbalimbali duniani ambapo nusu ya idadi hiyo wanafanyishwa kazi ngumu za sulubu hususan zile za migodini na hivyo kuhatarisha afya na maisha yao.
Papa: Kuwatumikisha watoto ni utumwa mamboleo Papa: Kuwatumikisha watoto ni utumwa mamboleo Reviewed by WANGOFIRA on 20:41:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.