IPO WAPI NGUVU YA BUNGE KWENYE MAAMUZI YA NCHI YETU?



NA, Abdul Nondo.

Mwanafalsafa wa kingereza John locke na  wa kifaransa  Baron DE Montesque, walikuwa wapiganaji wakubwa wa demokrasia walioibuka kipindi nchi za ulaya zikitawaliwa kiifalme yaani (absolute monarchy). Stuart dynasty Uingereza Chini ya Charles 1, James ll na Bourbon Monarchy Ufaransa Chini ya King Louis xvi.

wanafalsafa hawa Walikemea sana ujimilikishaji wa madaraka kwao wenyewe na Familia zao (hereditary system)  katika nchi za Uingereza na Ufaransa.

Hawakupendezwa na kauli na matamko ya baadhi ya viongozi wa kidekteta kama, kauli ya Charles 1 wa Uingereza katika kitabu chake (True Law of Free Monarchy) aliandika, 
"a monarchy is free from the control of Parliament, churchmen, laws and custom of past"".

Ukisoma maelezo haya ni wazi kuwa Charles 1 wa uingereza alikuwa Dikteta kwani katika nchi ya kidemokrasia bunge lipo kukosoa, kushauri na kuisimamia serikali. Je, nchi yetu ipo katka Hali gani  kwa Sasa?

Tanzania Sasa imeanza kutupilia mbali misingi yote ya kidemokrasia ambayo tumekuwa nayo siku nyingi. Katika awamu hii tumeshuhudia wabunge wakiadhibiwa kwa kuishauri na kuikosoa serikali, Yale yale kama ya Charles 1,"a monarchy is free from control of Parliament, churchmen, laws, and custom of past""ni wazi nchi yetu demokrasia imebanwa na bunge limenyang'anywa nguvu ya kuikosoa na kuiwajibisha serikali badala yake wabunge wana wajibishwa kwa kile kinachodaiwa makosa ya kinidhamu.

Nchi ya ufaransa katika utawala wa kifalme na kidekteta wa Bourbon monarchy uliokuwa chini ya King Louis wa XVI, aliwahi kutamka, 
'"Am the state and state is me something is legal because, l wish it".

Aina ya Udiktekta wa  namna hii unaitwa  "RULLING PRESIDENTS" Raisi ndiye anamiliki nguvu, na maamuzi yote hata yale ambayo yanafuata sheria, yaani anaona nchi hii mtawala ni yeye peke yake na ana uwezo wa kufanya na kuamua lolote alitakalo kwa kulion ani jema kwake.

Je, kauli  ya King Louis ina uhusiano gani na kauli za viongozi wetu?

Ni ukweli usiofichika kuwa kauli za King Louis zina uhusiano wa moja kwa moja na baadhi ya  kauli mbalimbali zitolewazo na kauli za viongozi wetu. Mfano mzuri ni tamko la serikali la kuhalalisha bunge kutooneshwa  mbashara (LIVE) kwa sababu aMBAzo mpaka leo hazina kichwa wala miguu.

Pia, Baron DE Montesque, Mwanafalsafa wa Kifaransa alipenda Nchi yake iwe na mgawanyo wa madaraka maana nchi isio na mgawanyo wa madaraka, hiyo ni nchi ya kidekteta.

Aliandika kitabu kitwaacho" The Spirit of Laws" aliezea juu ya umuhimu wa mgawanyo wa madaraka yaani "separation of power" akitaka mihimili ya dola yaani  bunge, mahakama na dola kufanya kazi pasipo kuingiliwa na muhimili mwingine.

Je, Tanzania hii inatekelezwa nchini kwetu?
Jibu ni  HAPANA, maana bunge ndilo lina kazi ya kuidhinisha matumizi ya fedha, ila kwasasa kinashuhudiwa ni dola(executive) ndio inajiidhinishia matumizi ya fedha. Ni wazi bunge imeporwa jukumu lake.

Ni wazi, utawala wa namna hii ni wa kupora demokrasia, Ndio maana Wana falsafa wa kubwa walipinga vikali Aina ya utawala huu (absolutism) huko Uingereza na ufaransa, hivyo, ni Zamu ya wasomi katika nchi hii kujua tunaelekea wapi Sasa
,

IPO WAPI NGUVU YA BUNGE KWENYE MAAMUZI YA NCHI YETU? IPO WAPI NGUVU YA BUNGE KWENYE MAAMUZI YA NCHI YETU? Reviewed by WANGOFIRA on 21:50:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.