POLISI WAZUNGUMZA BOMU LILILORUSHWA KWENYE NYUMBA YA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR

March 15 2016 kituo cha ITV kiliripoti taarifa kutoka visiwani Zanzibar ambapo ilidaiwa kuwa na taarifa za watu wasiojulikana kurusha bomu nyumbani kwa Kamishna wa jeshi la polisi Visiwani Zanzibar eneo la Kijichi.

Sasa taarifa niliyoipata ni kwamba nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame imeripuliwa  na kitu kinachosadikiwa kuwa  ni bomu na watu wasiojulikana  majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na  kujeruhi baadhi ya watu  waliokuwa wamelala  na kusababisha hasara kubwa.
Amesema tukio hilo linafanana lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya  uhalifu huo.
2110
Akizungumzia  matukio  mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema  Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa  katika vyombo vya sheria.
Kamishna Hamdani amewatoa hofu  wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo  mengi ya mijini na vijijini  ni  moja ya juhudi za kuimarisha  ulinzi  na kuhakikisha  uchaguzi huo utakuwa salama na amani.
Source:Full Shangwe
POLISI WAZUNGUMZA BOMU LILILORUSHWA KWENYE NYUMBA YA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR POLISI WAZUNGUMZA BOMU LILILORUSHWA KWENYE NYUMBA YA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI  ZANZIBAR Reviewed by WANGOFIRA on 09:16:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.