KIJANA USIBWETEKE TUMIA FURSA ILIYO KWENYE MAENEO YANAYOKUZUNGUKA
Na Fulgence Makayula
Suala la ajira limekuwa kilio cha mda mrefu sana miongoni mwa Watanzania wengi hasa vijana.
Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, lakini ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa kukosa ajira na fursa mbalimbali ili kujikwamua kimaisha. Wimbi kubwa la vijana wamekuwa wakiyahama makazi yao na kwenda mijini kwa kile wanachokiita, maisha” wakiwa na dhana kwamba mjini ndiko sehemu pekee ambako ni rahisi
kupata ajira, la hasha, maisha ya mjini yamekuwa tofauti sana na yale ambayo
vijana wengi wamekuwa wakiyafikiria na hatimaye wengi huishia kutangatanga tu
pasipo mafanikio.
Kuna fursa
nyingi sana vijina wanaweza kuji ajiri wenyewe na kujikwamua kimaisha, vijana
waishio bonde la Kilombero, Mkoani Morogoro wamepata Baraka kubwa ya kuwa na
eneo nzuri la shughuli za kilimo, mbali na shughuli za kilimo cha mpunga na
mahindi ambazo hufanywa na wakazi wa Kilombero, pia bonde hilo limeonekana kuwa
na rutuba iliyosafi sana kustawisha zao la tikitiki maji.
Zao hilo linapendwa na
watu wengi sana mkoani Morogoro na
sehemu zingine nchini, tokana na mahitaji yake katika mwili, kwa mfano, Tikiti maji mbali na kuwa na radha nzuri pia ni chanzo
kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A, inayosaidia kuboresha
afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; Vitamin C, inayosaidia kuboresha
kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi;
na vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini
kuwa nishati.
Tunda
la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga
za majani.
Ikiwa
familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasiam,
unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na
mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikiti
pia lina amino asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko
wa damu kwenye mishipa yake.
Kuna
faida nyingi sana ambazo wataalamu wanazidi kuzielezea kutoka katika tunda
hilo, hivyo kusababisha zao hilo
kuongezeka kwa soko lake. Kwahiyo hiyo ni fursa tosha sana kwa vijana wa Jimbo
la kilombero kujiajiri.
Zao
la tikiti lina hitaji jua la kutosha, maji mengi, na ardhi yenye rutuba na
hivyo vyote vinapatikana katika bonde hilo, tena zao hili linaweza kulimwa hata
mara nne kwa mwaka inategemeana na mbegu, pia endapo ukame utazidi pia unaweza
kulima kwa kumwagilia ambapo kila shina linahitaji lita kumi za maji, ambazo
utamwagalia asubuhi na jioni, laikini bonde la kilombero limebarikiwa kuwa na
chemchem nyingi sana za maji ambazo zimetoka kwenye mto kilombero
unaotenganisha wilaya ya Ulanga na kilombero hivyo zoezi la umwagiliaji sio
changamoto sana.
Ngoja
niwape mfano namna kijana anavyoweza kufaidika kutokana na zao hili la tikiti,
matikiti maji hukua haraka kama mimea mingine itambaayo ya jamii yake kama vile maboga, matango na
maskwash. Zao hili litaonekana gumu kidogo kama ni mara ya kwanza kuanza
kwasababu linahitaji umakini kiasi, ila pia ni zao jepesi sana kulimudu endapo
utazingatia taratibu zake za kilimo na pia litakuwa zao kombozi kwa vijana
wenye nia ya kujikwamua kimaisha, udongo wa bonde la kilombero lina rutuba
nzuri na lina udongo unaotuhamisha maji,hivyo linatumia mbolea kidogo sana
kutoka viwandani, ili kuweza kupata mavuno makubwa kutoka zao hili unaweza
kuongeza kutumia mbolea kidogo za samadi, na za viwandani zenye naitrojen na
potasiam ili kuimarisha zaidi mazao yako.
Zao
la tikiti linaanza kukomaa kuanzia siku ya 80-120 kulingana na aina ya mbegu,
zingine huanzia kuvunwa siku ya 54-60.
Kwa mfano ukipanda mbegu aina ya ``sugar baby”
unaweza kuvuna baada ya siku 60 tangu
siku ya 3-5 za kukaa ardhini, kwahiyo kwa mwaka unawezsa kulima hata mara 4. Na
ukipanda kwa nafasi ya mita 2 kwa 2 na kila shimo ukiweka mbegu mbili ambazo
zinatoa wastani wa matunda matano.
Hivyo
kwa nafasi hiyo kwa ekari moja endapo ukaweza kupanda mashimo 200-240, kwa makadilio ya
chini.
Idadi
ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari ( 200x5x1=1000 )
Mapato:
Wastani wa shilingi 1000 kwa tikiti x idadi ya tikiti kwa eneo la ekari 1, ( 1000
x 1000 = 1,000,000 ) hiyo ni kilimo cha mara
moja tu, je, ukilima mara mbili na zaidi utakuwa wapi?
Huo ndio uhalisia wa zao hilo na
kama kijana ukaitumia vizuri fursa hii ni lazima ufikie malengo uliyo jiwekea,
na zaidi sana kama utaendana na kasi ya sera ya HAPA KAZI TU, na kweli ukawa
unajituma katika kazi, basi kuna uwezekano mkubwa sana wa kufanya mabadiliko
juu ya maisha yako badala ya kukaa vijiweni na kulalamikia selikari haitoi
ajira kwa vijana.
Makala
haya yameandikwa na Fulgence Makayula mwanafunzi wa Shule kuu
ya uandishi wa Habari na Mwasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaam.
Anapatikana kwa mawasilaano ya 0655887798.
KIJANA USIBWETEKE TUMIA FURSA ILIYO KWENYE MAENEO YANAYOKUZUNGUKA
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:41:00
Rating:
No comments: