SOKA LA TANZANIA LITAENDELEA IKIWA LITAZINGATIA YAFUATAYO.



Na Shaaban Maulidi (Shablil President)

Bila Shaka kwa miezi takribani mitatu hivi iliyopita huenda maneno yaliyokuwa yakitamkwa sana katika vinywa vya watanzania labda tuseme Mabadiliko, Hapa kazi tu ,Ukawa, CCM, Uchaguzi mkuu, October 25, tutawakata na mengine mengi lakini hata majina ya watu hususani wagombea hasa nafasi ya urais hapa nawazungumzia Mh. Edward Lowassa na John Pombe Magufuli ambapo tutakubaliana sote kuwa ndiyo yalikuwa yakitatajwa na kuandikwa kwa kiasi kikubwa iwe kwenye magazeti ama mitandao ya kijamii.

Lakini kwa siku za hivi karibuni tumekuwa tukisikia neno Taifa Stars likitajwa sana huenda kwa sababu ndilo jina la timu ya Taifa ya Tanzania ambayo mwishoni mwa wiki hii tumeshuhudia ikishuka dimbani ili kusaka nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya makundi na hatimaye kushiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo kikubwa kabisa duniani.

Kama ungefuatialia kwa umakini maneno ya watawala wetu ngazi ya kitaifa sambamba na wale wa kimichezo, hapa nazungumzia Shirikisho la Soka Tanzania TFF. Ungegundua kuwa viongozi hawa Wana nia ya dhati ya kulikwamua taifa hili kimichezo lakini badala yake imekuwa kinyume.

Kumekuwa na utaratibu mbovu hususani kwenye maandalizi ya timu kwa sababu sikuona hatua zozote stahiki zilizochukulia ili kuweza kufanikisha hili. Tanzania imekuwa ni nchi ya kuwateua na kuwaweka wachezaji pamoja ili wakacheze mpira pasipo na maandalizi yaliyo na Tija.

Baada ya kichapo cha goli 7 -  0 tulichokipata kutoka kwa Algeria ndipo imethibitisha kuwa Taifa Stars haikuandaliwa kimapambano. Katika mchezo wa awali tulijitahidi kucheza kandanda saafi lililomvutia kila mtazamaji na kuamsha matumaini ya watanzania wengi waliokuwa wamepoteza dhidi ya Timu hiyo, lakini kwa kitendo cha Stars kuongoza kwa goli 2 -  0 mbele ya Algeria hadi dakika ya 70 kilithibitisha kuwa hata Tanzania tunaweza. Lakini dakika tatu pekee zilibadilisha hali ya mchezo na fikra mawazo shamrashamra na matumaini ya watanzania mara tu baada ya Algeria kusawazisha magoli hayo na kuufanya mchezo kukamilika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili.

Kosa lililooneka kwa wachezaji na hata benchi la ufundi ni kushindwa kumtambua mpinzani wetu.Kitendo cha wachezaji kujisahau kuwa wanacheza na Algeria ambao kwa viwango vya soka wametuzidi mbali kuanzia vile vya CAF mpaka vya FIFA. Waliinekana wazi wamerizika na matokeo na kuanza kucheza mchezo ambayo ulikuwa si wa kiushandani tena kama ule wa awali katika kipindi cha kwanza hili lilikuwa kosa kubwa sana,walipunguza Kasi ya mchezo, hawakuwa na uchu w kukaba vilevile hata ile hali ya kuonyesha kutaka goli jingine haikuwepo ndipo kutoa mwanya kwa Algeria ambayo walionekana mwanzoni walikuwa wakiusoma mchezo na kutafuta hata sare ili nyumbani kwao wakafanya kweli.

Mchezo ambao umeingia katika rekodi za medani ya Soka nchini hapa tangu mwaka 1964 baada ya Tanzania kukubali kichapo cha mara ya kwanza tangu muda huo kwa kuruhusu mabao 7 dhidi ya Algeria. Kichapo hiki sio tu kinasikitisha bali pia kinatia huruma na kimeumiza nyoyo za watanzania wengi wenye mahaba na mchezo huo unaoongoza kwa kupendwa zaidi duniani. Sio kwamba mimi ninasikitika kafungwa hapana kwa sababu natambua kuwa katika soka kuna matokeo ya aina tatu moja wapo yakiwa ni hayo. Lakini hali ambayo wachezaji wengi wa Tanzania waliyokuwa nayo na kupelekea dhahama hiyo ya magoli ikitishukia mbele ya Nyota wetu wa Kimataifa Mbwana Samatha.

Stars walioonekana kukosa kujiamini kwa kiasi kikubwa huku wakiwa na hofu, kukosa umakini na uhakika wa kile wanachokifanya, ndipo ikapelekea kutoa mwanya kwa Mbweha hao wa Jangwani kufanya watakalo na hatimaye Tanzania kupata kichapo cha mbwa mwizi cha Jumla ya mabao 7 -  0.

Kimsingi na kiuhalisia Algeria ni timu bora sana kwa upande wa soka hasa barani Afrika lakini na ulimwenguni pia wenzetu wametuzidi mbali.Sababu iliyofanya sisi tuonekane dhaifu ni kutowekeza katika soka kama wafanyavyo wengine.

Nionavyo mimi sasa Serikali ya Tanzania kupitia wizara husika haina budi kuandaa vijana wataokuja kusakata kabumbu the kuiletea nchi heshima katika medani za kimichezo hususani anga za kimataifa. Wachezaji wetu wameoneka kukosa uzoefu wa Kimataifa, kutokuwa na umakini na hii inasabishwa na mbinu hafufu za kiufundi. Wachezaji wanatakiwa waandaliwe tangu wakiwa watoto.

Wataandaliwa vipi kwanza ni kuanzisha mashindano tatakayowahusisha wenyewe ili wauzoee mpira kutokea utotoni pia zijengwe Shule /Vyuo /vituo vya kimichezo vya watoto ili waweza kupata wasaa wa kutosha wa kujifunza soka.

Tatizo jingine tulilonalo ni wachezaji wetu kukosa uzoefu wa Kimataifa, ni wazi kuwa Tanzania tuna uhaba wa wachezaji wa Kimataifa ukilinganisha hata na wapinzani wetu Algeria ambao wengi wa wachezaji wao wanachezaji soka la kulipwa Ulaya huku Tanzania tukiwa hatuna mchezaji hata wa dawa wa namna hiyo. Mimi nadhani ni wakati sasa wa kuweka uhusiano mzuri na nchi za wenzetu ambao wamepiga hatua kimichezo hususani Soka. Tukishaweka huu uhusiano tuwe na utaratibu wa kuwapeleka vijana wetu wakajifunze soka katika vituo vya kimichezo vya wenzetu kwa mfano Uingereza, Hispania, Ufaransa, Brazil n.k.

Kama vijana wakipata fursa ya kwenda miongoni mwa nchi hizo ili kujifunza na kukuza uwezo wao wa kisoka tena kwa udhamini wa serikali wanaweza kupata fursa ya kasajiliwa na vilabu vya huko ha hatimaye kucheza soka la Kimataifa ili timu yetu ya Taifa iwe inaundwa na wachezaji wenye uzoefu Kimataifa na hatimaye kupata timu ya Taifa bora yenye mafanikio.

Narudia tena ili tuweze kujenga Taifa Stars bora hatuna budi kuwekeza kwa watoto na vyama vijana wapate mafunzo ya kutosha ndani na nje ya Tanzania.
SOKA LA TANZANIA LITAENDELEA IKIWA LITAZINGATIA YAFUATAYO. SOKA LA TANZANIA LITAENDELEA IKIWA LITAZINGATIA YAFUATAYO. Reviewed by WANGOFIRA on 22:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.