TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
 (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

Maombi mapya ya Udahili
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 5 Oktoba 2016 hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.

Maombi ya Uhamisho
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo, ushindani na alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi zitatolewa hivi punde.

Hatua za kuomba uhamisho:
  1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili.
  2. Bofya kitufye kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
  3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
  4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
  5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
  6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
  7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh. 30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho. Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
  8. Bofya kitufye kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha maombi”.
  9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.
Jinsi ya kulipia (Malipo yatafanywa kwa M- pesa tu)
  1. Piga *150*00#
  2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
  3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
  4. Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
  5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
  6. Weka kiasi (e.g.30,000/=)
  7. Weka namba ya siri
  8. Bonyeza 1 kuthibitisha.
Angalizo (Disclaimer)
  1. Kuhama chuo na kozi si lazima.
  2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
  3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
  4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja
  5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (15 Oktoba 2016).
  6. Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo mkubwa wa kukubaliwa kuhama.
  7. Maombi yatakayo tumwa kwa barua au barua pepe hayatoshughulikiwa.
Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
Tarehe: 02 Octoba, 2016
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 Reviewed by WANGOFIRA on 03:48:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.