Profesa Mubofu Makamu Mkuu wa Chuo Mpya UDOM.
Na Paschal
Dotto-MAELEZO
Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM) Rais Mstaafu (Awamu ya Tatu), Mhe. Benjamin William Mkapa ametangaza
uteuzi wa Profesa Egid Beatus Mubofu
kuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Profesa
Idris Suleiman Kikula.
Uteuzi huo
umetangazwa rasmi leo tarehe 5, Machi 2018 kupitia taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari na ofisi ya Mkuu wa UDOM,
Mhe. Benjamin Mkapa.
Kabla ya uteuzi huo Profesa
Mubofu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na kabla
ya hapo alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, uteuzi wa Profesa Mubofu unaanza rasmi tarehe 17 Machi, 2018.
Profesa Idris Kikula
ni miongoni mwa wanazuoni waandamizi wanaoheshimika ndani na nje ya nchi kitaaluma kwa kushiriki katika
tafiti mbalimbali za kisayansi na kijamii
Ameshiriki katika
tafiti hizo kwa kushirikiana na taasisi nguli za kitafiti hapa nchini kama REPOA, pamoja na taasisi ya UONGOZI.
UDOM ndio chuo kikuu
pekee chenye uwezo mkubwa wa kuchukua wanafunzi wengi hapa nchini na Afrika
Kusini mwa jangwa la Sahara na inakadiriwa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi takriban
40,000, pia kina eneo la ukubwa wa hekari zaidi ya 6000.
Profesa Mubofu Makamu Mkuu wa Chuo Mpya UDOM.
Reviewed by WANGOFIRA
on
19:43:00
Rating:
No comments: