AUAWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Idd Selemani, (40), Mkazi wa Jineri katika Manispaa ya Singida ameuwa kwa kuchomwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na Mtuhumiwa aitwaye Khalid Rajabu, (45), fundi viatu na Mkazi wa Jineri baada ya mtuhumiwa huyo kumkuta akiwa na mke wake chumbani kwake.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida SSP Isaya Mbughi amesema tukio hilo  limetokea jana majira ya saa majira ya saa 9:30 alasiri.


Ameeleza kuwa  mbinu aliyoitumia mtuhumiwa kufanya tukio hilo kuwa ni kumvizia marehemu akiwa na mke wa mtuhumiwa aitwaye Mariam Ibrahimu, (25) mkazi wa Jineri wakiwa chumbani kwa mtuhumiwa ambapo mtuhumiwa huyo aliingia chumbani kwake kisha kufunga mlango na kuanza kumshambulia Marehemu na kumsababishia majeraha kisha kufariki muda mfupi wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa Singida.


Amesema chanzo cha mauaji hayo kuwa ni wivu wa kimapenzi.

 Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa Khalid Rajabu na mke wake kwa mahojiano na baada ya mahojiano kukamilika watuhumiwa watafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Kaimu Kamanda ametoa wito kwa Wananchi wote kwa kuwataka kuacha kujichukulia sheria mkononi bali watoe taarifa vituo vya Polisi pindi wanapopata migogoro yenye utata ili kuchukua hatua za kisheria na kuongeza kuwa wazazi/wanandoa wanatakiwa kuwa waaminifu katika ndoa zao ili kuepusha migogoro inayoweza kuleta athari.
Chanzo-MACHIBYA  blog
AUAWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU  AUAWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU Reviewed by WANGOFIRA on 22:12:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.