KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO SHINYANGA LAKARABATI JENGO LA WAZEE KITUO CHA KOLANDOTO
Kanisa la Waadventista Wasabato mjini
Shinyanga kupitia idara ya vijana limekarabati jengo moja lenye vyumba
sita katika kambi ya kulelea Wazee Kolandoto katika manispaa ya
Shinyanga baada ya kufika katika kituo hicho na kujionea changamoto ya
ubovu wa majengo ambayo ni hatari kwa maisha ya wazee hao ambao sasa
wapo 18.
Akizungumza wakati wa kukabidhi jengo
hilo leo Jumamosi June 24,2017,Mratibu wa Idara ya Vijana Kanisa
Waadventista Wasabato Kanda ya Shinyanga Wilson Mjinja alisema jengo
hilo lilikarabatiwa kuanzia Mwaka 2016 hadi 2017 kwa gharama ya shilingi
milioni 1.8 ambapo vijana wa kanisa hilo walishiriki kwenye ukarabati
ili kupunguza gharama za ukarabati.
Akipokea jengo hilo kwa niaba ya serikali ,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Josephine Matiro amelilipongeza kanisa hilo kwa moyo waliouonyesha
kukarabati jengo hilo kutokana na wazee hao kukabiliwa na ubovu wa
majengo ambayo ni hatari kwa maisha ya wazee hao.
Matiro alitoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuwatatulia
changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee hao ikiwamo na kukarabati
majengo mengine yaliyosalia ili waishi mahali salama.
Naye Askofu Kanisa la Wasabato Jimbo Kuu Kaskazini Mwa Tanzania, Dk.
Godwin Yakundaya alisema dini safi ni ile ya kusaidia watu wenye uhitaji
na siyo kuwa na majengo mazuri na vyombo vizuri vya muziki bali ni
kusaidia pia watu ambao wanaishi maisha magumu.
Dk. Yakundaya alisema dhana ya dini safi ndiyo sababu iliyowapelekea
kuguswa kuwasaidia wazee hao kwa kuwakarabatia majengo ili waishi mahali
salama na kubainisha kuwa huo ni mwanzo tu wataendelea kutoa huduma kwa
wazee hao zaidi.
Mbali na kanisa hilo kukabidhi jengo walilokarabati kwenye kambi hiyo ya
wazee pia wametoa zawadi ya chakula ambayo ni mchele kilo 120, Mbuzi
mmoja,mafuta ya kupikia,boksi la sabuni la kufulia pamoja na vitabu vya
kidini kwa ajili ya kusoma neno la Mungu.
Askofu wa kanisa la Wasabato jimbo Kuu Kaskazini mwa Tanzania Dk.
Godwin Yakundaya akisoma neno la Mungu katika kambi ya wazee Kolandoto
ambapo alisema dini safi ni ile ya kusaidia watu wenye uhitaji.
Askofu wa kanisa la Wasabato jimbo Kuu Kaskazini mwa Tanzania Dk. Godwin Yakundaya akizungumza katika kambi ya wazee Kolandoto.
Mratibu wa idara ya vijana kanisa la Wasabato kanda ya Shinyanga Wilson
Mjinja akizungumza katika kambi ya wazee Kolandoto ambapo alisema jumla
ya shilingi milioni 1.8 zimetumika kukarabati jengo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifungua mlango wa chumba
kimoja katika kituo cha kulelea wazee Kolandoto katika manispaa ya
Shinyanga lililokarabatiwa na kanisa la Waadventista Wasabato kama
ishara ya kulipokea jengo hilo kwa niaba ya serikali mkoani Shinyanga
.Mkuu huyo wa wilaya alipongeza jinsi lilivyokarabatiwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka ndani ya chumba kimoja cha jengo hilo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua jengo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya
kupokea jengo hilo ambapo aliwaomba wadau wengine wa maendeleo
kujitokeza kukarabati majengo yaliyosalia katika kituo hicho
Hili miongoni mwa majengo yaliyochakaa katika kituo cha kulelea wazee
Kolandoto,ambalo linahitaji kukarabatiwa au kubomolewa lijengwe jengo
jingine
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikabidhi zawadi ya
chakula msimamizi wa kambi hiyo ya wazee Sophia Kang'ombe ambavyo
vimetolewa na waumini wa kanisa la Wasabato mjini Shinyanga.
Wazee wa kambi hiyo na watu mbalimbali waliofika katika kambi hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwenyekiti wa kambi ya wazee Kolandoto Samwel Maganga akipokea zawadi ya mbuzi kwa niaba ya wazee wa kambi ya Kolandoto
Mwenyekiti wa kambi ya wazee Kolandoto Samwel Maganga akipokea zawadi
ya mbuzi ambapo alilishukuru kanisa la Wasabato kwa kuwakarabatia jengo
hilo na zawadi ya chakula ambacho watakitumia hasa kwenye sikukuu ya Eid
mwezi huu.
Picha zote kwa hisani ya Marco Maduhu
KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO SHINYANGA LAKARABATI JENGO LA WAZEE KITUO CHA KOLANDOTO
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:42:00
Rating:
No comments: