Kamanda Sirro awataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi badala yake waviachie vyombo husika ili viweze kufanya kazi yake.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari. Amesema kuwa wananchi kujichukulia sheria mikononi pindi wawakamatapo watuhumiwa ni kinyume cha sheria hivyo wanatakiwa kuacha mara moja tabia hiyo.

“Ni vyema wananchi wakaacha  tabia ya kujichukulia sheria mikononi ili vyombo usika vifanye kazi yake,”amesema Sirro.

Aidha, amesema kuwa wananchi kuwauwa watuhumiwa ni kosa kisheria kwani watakao bainika kufanya hivyo sheria kali dhidi yao zitachukuliwa.

Hata hivyo, ameongeza kuwa ni bora wananchi waache tabia hiyo ya kujichukulia sheria mikononi kwani vyombo husika kama Polisi na Mahakama vipo kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kamanda Sirro awataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi Kamanda Sirro awataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi Reviewed by WANGOFIRA on 00:34:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.