Zlatan Ibrahimovic: Mambo 14 usiyofahamu kuhusu yeye

Mwaka 2014, katika mahojiano na gazeti la The Guardian, Ibrahimovic alielezea kwamba anakumbuka alipokuwa mtoto baba yake alitoa akiba yote ya pesa alizokuwa nazo wakaenda dukani ili akamnunulie kitanda, baada ya kununua kitanda hicho wakajikuta hawana pesa za kulipia usafiri wa kukipeleka nyumbani, kwahiyo ikawabidi kukibeba wao wenyewe!

“Tulikibeba mimi na baba mpaka nyumbani. Nilifurahi tulivyokibeba. Kuna kipindi alitoa mshahara wake wote ili niweze kwenda kwenye kambi ya mazoezi. Alijua akinipa hataweza kulipa kodi ya nyumba, lakini alinipa pesa hiyo ili niende kambini.”
Yafuatayo ni mambo 14 ambayo huyajui kuhusu Zlatan Ibrahimovic a.k.a. Ibracadabra:
14. Akiwa na miaka 10 aliingia uwanjani kutoka benchi na kufunga magoli 8!
Akiwa anachezea klabu yake ya mtaani ya FBK Balkan akiwa umri wa miaka 10, Zlatan alichelewa kufika uwanjani kwenye mechi kwakuwa alikuwa anaishi mbali na alikuwa akienda uwanjani kwa baiskeli. Aliingizwa uwanjani kipindi cha pili wakati timu yake ipo nyuma kwa kufungwa magoli 5-0. Ibrahimovic akabadili matokeo ya mchezo huo kichwa chini miguu juu baada ya kufunga magoli 8 – ndio, magoli 8, yote katika kipindi cha pili tu, na kufanya washinde mchezo huo kwa magoli 8-5. Hapo ndipo jina la utani “The Zlatan” lilipozaliwa rasmi na dunia nzima ikaanza kufatilia kipaji cha hali ya juu cha bwana mdogo huyu.
13. Hataki kufanyiwa majaribio kabla ya kumnunua
Related image
Kwenye mahojiano aliwahi kuulizwa kwanini hakusajiliwa na Arsene Wenger kuichezea klabu ya Arsenal alipokuwa kijana, jibu lake lilikuwa ni kama ifuatavyo; “Zlatan hafanyiwi majaribio.” – alisema alipoulizwa kuhusu Wenger alipomtaka ujanani kwake.
“Ukininunua mimi, ujue kuwa unanunua gari aina ya Ferrari. Ukitaka kuendesha Ferrari unajaza petroli kwenye tenki, unatafuta barabara ya lami ilipo na unakanyaga mafuta mpaka mwisho. Guardiola alinijaza dizeli badala ya petroli, halafu akanipitisha barabara ya vumbi. Alitakiwa kununua Fiat, sio Ferrari.” – alisema alipoulizwa kuhusu uhusiano wake mbovu na kocha Pep Guardiola, kipindi hicho Jose Mourinho alikuwa msaidizi wa Pep Guardiola.
12. Mfungaji bora wa timu ya Taifa ya Sweden
Image result for zlatan scoring for sweden
Zlatan Ibrahimovic alizaliwa nchini Sweden, baba yake ni raia wa Bosnian na mama raia wa Croatia, ikimaanisha angeweza kuchagua kuchezea timu yoyote ya Taifa kati ya hizo mbili kwenye mashindano ya kimataifa. Alichagua Sweden kwa sababu ndipo alipozaliwa na kukua.
Yawezekana huo ulikuwa mbovu kwakuwa nchi hiyo imefuzu mara mbili tu katika mashindano matano ya mwisho ya kombe la dunia, lakini hawezi kubebeshwa lawama kwa hilo. Amejaribu kwa nguvu zake zote kuibeba timu yake ya Taifa! Yeye ndiye mfungaji bora wa timu hiyo akiwa na magoli 62 kwenye timu ya Taifa kabla ya kustaafu.
11.Jina lake limeingizwa kwenye Kamusi nchini Sweden
Image result for Zlatanera in swedish dictionary
Zlatan ni shujaa wa nchi ya Sweden kiasi kwamba jina lake limeongezwa kwenye kamusi inayotumia lugha ya nchi hiyo! Mwaka 2012, Baraza la Lugha ya Kiswidi lilitambua rasmi neno ‘Zlatanera’ litumike rasmi katika lugha yao. Neno hili linatokana na jina la mchezaji huyo.
Neno ‘Zlatanera’ linamaanisha kumiliki au kufanya jambo kwa ufundi au uwezo wa hali ya juu sana!
10. Mgahawa nchini Ufaransa una baga (burger) yenye jina lake
Image result for zlatan burger
Ibrahimovic alipata mashabiki wengi nchini Ufaransa hasa baada ya kuhamia klabu ya PSG, na walikuwa wengi kiasi cha kufanya mgahawa mmoja nchini humo kuwa na aina maalumu ya baga yenye jina la mchezaji huyo. Mgahawa huo unaoitwa Doddy’s, upo katika mitaa ya Boulogne-Billancourt. “Le Zlatan” ndio jina la baga hiyo na mmiliki wa mgahawa anasema kuwa ndiyo “inayopendwa zaidi” na wateja wake kama ambavyo Ibra anapendwa na mashabiki zake.
9. Anapenda filamu ya Scarface
Image result for scarface
Zlatan anasema kuwa filamu anayoipenda zaidi ni Scarface na huwa anaitazama mara mbili au tatu kila mwaka. Pia ameshawahi kutangaza kuwa kama akitaka kumualika mtu yeyote yule ili ale naye chakula cha jioni, basi mtu huyo lazima atakuwa Al Pacino, Muigizaji Mkuu katika filamu hiyo ya Scarface.
Kama kuna muigizaji atataka atengeneze filamu kuhusu maisha ya Ibra, basi Ibra mwenyewe atamchagua Pacino kwakuwa anasema ndio mtu pekee atayeweza kuigiza nafasi yake vizuri.
8. Uwanja wa mchangani aliojifunzia soka ulikarabatiwa kwa heshima yake
Image result for zlatan court
Ingawa yaweza kuonekana kwamba muda wote anafanya mambo kwa ajili ya sifa, Ibrahimovic hasahau alipotoka. Alipokuwa mtoto alikuwa akijifunza soka katika uwanja ambao awali ilikuwa bustani ya mama yake. Baada ya kuwa mchezaji wa kulipwa, mwaka 2007 Zlatan akidhaminiwa na kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike waliutengeneza upya uwanja. Uwanja huo ambao kwa sasa una uzio umepewa jina la “Uwanja wa Zlatan”, na utawezesha kizazi kipya kujifunza mchezo wa soka katika mazingira bora zaidi ya yale aliyojifunzia mcheza soka huyo wa kimataifa alipokuwa mtoto. Uwanja huu una ujumbe usomekao: Hapa ndipo ulipo moyo wangu. Hapa ndipo ilipo historia yangu. Hapa ndipo ulipoanzia mchezo wangu. Upeleke mbali, Zlatan.”
7. Kuna sanamu lake kwenye makumbusho ya jijini Paris
Related image
Zlatan amekuwa ‘akitukuzwa’ katika makumbusho ya Musée Grévinjijini Paris, Ufaransa kwa kuwa na sanamu lake. Sanamu hili linalomuonesha anashangilia kwa kuinua mikono yote ikielekea mawinguni (aina ya ushangiliaji anayoipenda zaidi). Katika makumbusho hii mchezaji mwengine ambaye si Mfaransa kuwekewa sanamu ni Pele wa Brazil, kwahiyo amepewa heshima ya kipekee sana. Hii inaonesha ni kwa jinsi gani amekuwa na mchango mkubwa kwa jiji la Paris na kwa nchi ya Ufaransa toka ajiunge na klabu ya PSG mwaka 2012.
6. Aliwapa zawadi wachezaji wenzake wa PSG toleo maalumu la ‘Xbox One’
Image result for zlatan giving psg players xbox one
Muda mfupi baada ya kushindwa kufuzu kwenda mashindano ya Kombe la Dunia, Zlatan aliwashangaza wachezaji wenzake wa PSG kwa kuwapa zawadi ya kifaa cha michezo ya video cha Xbox One (toleo maalumu), kila kimoja kikiwa na jina la mchezaji husika na namba ya jezi yake – bila kusahau sahihi ya Zlatan. Ibrahimovic ni balozi pekee wa vifaa vya Xbox One nchini Ufaransa, ikimruhusu kuwapa wachezaji wenzake zawadi hiyo ya kipekee aliyoibuni.
5. Ni mchezaji pekee kufunga kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na timu sita tofauti
Zlatan amedhihirisha kuwa ni mshambuliaji wa kiwango cha kipekee bila kujalisha jezi aliyoivaa kwa kufunga katika mashindano makubwa zaidi Barani Ulaya katika ngazi ya vilabu akiwa na timu sita tofauti. Hili linaashiria mambo mawili, kwanza yeye ni mfungaji wa kiwango cha juu kabisa ambaye anaweza kukaa chini ya walimu tofauti, pia inaonesha kuwa timu zote za juu katika ligi za Ulaya zinamuhitaji. Katika Klabu Bingwa, amefunga magoli akiwa na klabu za Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan na PSG. Ingawa amezifungia magoli mazuri sana, lakini mpaka sasa bado hajalibeba kombe hilo.
4. Alitabiri hatma ya maisha yake akiwa utotoni
Alipokuwa na miaka 16, Zlatan akijibu mtihani wake wa somo la Kiingereza, katika swali lililoulizwa: “Utakuwa nani baada ya miaka mitano?.”
Alichokiandika Zlatan kujibu swali hilo ni kwamba “nitakuwa mchezaji wa kulipwa wa mpira wa miguu nchini Italia, nitalipwa pesa nyingi sana, nitakuwa namiliki nyumba ya kifahari karibu na bahari na nitakuwa tajiri mkubwa sana.”
Haya aliyajibu akiwa na miaka 16!
3. Alikuwa mwizi wa baiskeli utotoni
Zlatan amekulia katika sehemu ya watu maskini mjini Malmo, Sweden na mara nyingi alikuwa akiiba baiskeli za watu na kuendesha kilomita 5 kwenda na kurudi mazoezini.
Alipokuwa mdogo, alikuwa na baiskeli aliyokuwa anaipenda sana lakini ikaibwa. Kuanzia hapo na yeye akawa mwizi wa baiskeli kulipiza kisasi …
Alipokuwa klabu ya Malmo, Zlatan alienda mazoezini na baiskeli ambayo aliiba, alipomaliza mazoezi akakuta imeibwa. Zlatan akaamua kuiba baiskeli nyingine na kurudi nayo nyumbani.
Habari zilizopo ni kwamba alishawahi kuiba hadi baiskeli ya Meneja wa timu yake kipindi fulani. Ilibidi wachezaji waliokuwa wanachezea timu ya vijana waitwe kwenye kikao na ndipo Zlatan alipopewa somo refu baada ya kugundulika yeye ndiye aliyeiba baiskeli hiyo. Zlatan alisema sababu ilikuwa ni kuhitaji usafiri kwakuwa uwanja wa mazoezi ulikuwa mbali.
2. Ronaldo de Lima ndio shujaa wa Zlatan
Image result for zlatan and de lema
Ibrahimovic amekuwa akimtukuza ‘The Phenomenon’ Ronaldo Luis Masouza de Lima, mshambuliaji wa zamani raia wa Brazil, na mara zote huwa anamuelezea kama mchezaji bora zaidi “kwa wakati wowote”
Ibra alihamia klabu ya Inter Milan mwaka 2006 akifuata nyayo za shujaa wake huyo. Alipokuwa klabu ya Inter ndipo alikutana na bosi wa sasa wa Man United, Jose Mourinho.
1. Ana mikanda miwili ya rangi nyeusi kwenye mchezo wa kupigana aina ya Taekwondo
Related image
Kwa aina ya tabia na uchezaji wake, Ibrahimovic huwa anajikuta kwenye mabishano na ugomvi kati yake na wachezaji wa timu pinzani. Huyu ni mchezaji ambaye hata wewe usingetaka awe mpinzani wako sehemu yoyote ile kwakuwa ana uwezo wa kupigana kama ukimshinda kwenye kubishana. Uwezo wake mkubwa wa kupigana ndio unaomuwezesha kuruka mateke ya juu ingawa ana umbile kubwa.
Kuna vitu viwili ambavyo Zlatan anavipenda kupita kiasi: kwanza kufunga magoli ya ajabu ya tikitaka yanayozidi kimo cha mtu, na pili kuwapiga mateke ya kichwa wachezaji wenzake kama masihara wakiwa mazoezini.
Zlatan ni mtaalamu wa kupigana, ana mkanda mweusi wa mchezo wa kupigana aina ya Taekwondo ambao hutumia zaidi mateke alioupata nchini Sweden akiwa na umri wa miaka 17 mjini Malmo, pengine ndio sababu anapenda sana kuwapiga wachezaji wenzake mateke ya kichwa wawapo mazoezini.
Mwaka 2010 akiwa anachezea klabu ya AC Milan ya Italia, alipewa mkanda mweusi wa heshima na Shirikisho la Mchezo wa Taekwondo nchini humo. Aliwahi kusema kuwa kama asingekuwa mcheza soka, basi angekuwa mpiganaji wa kimataifa katika mchezo huu.
Zlatan Ibrahimovic: Mambo 14 usiyofahamu kuhusu yeye Zlatan Ibrahimovic: Mambo 14 usiyofahamu kuhusu yeye Reviewed by WANGOFIRA on 19:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.