WATU WENYE VIPARA WASHEREHEKEA SIKUKUU YAO


Wenye vipara wakishiriki katika mchezo wa kuvutana na kamba Japan
***
Zaidi ya wanaume 30 wenye vipara kichwani nchini Japan wanaadhimisha siku kuu yao ya kila mwaka inayoshirikisha mchezo wa kuvuta kamba.

Klabu hiyo ya wenye vipara inawajumuisha wananchama 65 kutoka maeneo tofauti nchini tangu ibuniwe 1989.

Lengo ni kuwahamasisha watu zaidi kuhusu watu wenye vipara

Mwanachama wa watu wenye vipara akishiriki katika mchezo wa kuvutana kwa kutumia kamba Japan

Mwenyekiti wa klabu hiyo Teijiro Sugo mwenye umri wa miaka 70 alisema kuwa matumaini ni kwamba klabu hiyo ingewavutia wanachama zaidi na kuwa kubwa zaidi.

''Nawataka wanaume wote walio na upara duniani kukongamana hapa ili kuanzisha michezo ya olimpiki'',alisema.
WATU WENYE VIPARA WASHEREHEKEA SIKUKUU YAO WATU WENYE VIPARA WASHEREHEKEA SIKUKUU YAO Reviewed by WANGOFIRA on 20:57:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.