Rais Magufuli na Mkewe wachangia Sh. Mil 5 Matibabu ya Mtoto Haidari Bonge anayeotwa na nyama kichwani


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wametoa mchango wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge mwenye umri wa miaka 7 anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, mdomoni na machoni.

Mtoto huyo anayeishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam alianza kuotwa na nyama miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo mara baada ya kutazama kipengele cha Hadubini “Habari kwa Kina” kilichorushwa hewani katika taarifa ya habari saa 2 usiku na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  jana tarehe 03 Desemba, 2016.

“Mimi na Mke wangu tumeguswa na tatizo linalomkabili Mtoto Hidari Bonge na tumeamua kuchangia Shilingi Milioni 5 kutoka kwenye mshahara kwa ajili ya kuchangia matibabu yake.

“Pia tunatoa pole kwake na kwa familia yake ambayo imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuhakikisha anapatiwa matibabu kwa kipindi kirefu cha miaka 7 sasa” amesema Rais Magufuli.

Mchango huo utakabidhiwa leo  tarehe 04 Desemba, 2016.
Rais Magufuli na Mkewe wachangia Sh. Mil 5 Matibabu ya Mtoto Haidari Bonge anayeotwa na nyama kichwani Rais Magufuli na Mkewe wachangia Sh. Mil 5 Matibabu ya Mtoto Haidari Bonge anayeotwa na nyama kichwani Reviewed by WANGOFIRA on 19:54:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.