BREAKING NEWS: ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA GEREZANI KISONGO ASEMA LEMA ANA ARI YA MAPAMBANO


Kiongozi wa Chama cha Act wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, leo amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini CHADEMA Godbless Lema gerezani kisongo Arusha.

 GodBless Lema
katika ukurasa wake wa Facebook leo Zitto ameandika ifuatavyo 

AMEANDIKA ZITTO KABWE

''Leo Ijumaa disemba 2/2016 nimepata fursa ya kumsalimu ndg. G Lema, mbunge wa Arusha Mjini Katika Gereza Kuvu la Arusha. Nimemtembelea Kama mbunge mwenzangu na kumhakikishia solidarity katika harakati Za kutafuta na kulinda Haki.

Lema ana ari kubwa ya mapambano. Anasikitishwa Sana na ukiukwaji mkubwa wa Haki na mahakama kuonekana kuendeshwa na Serikali. Yeye ameona Ni bora akae ndani Mpaka hapo Dola itakapopenda kumpa dhamana. Kosa lake lina dhamana na hakimu alimpa dhamana. 

Ameomba tutazame mahabusu wengi wanaokaa ndani miaka Mingi bila kesi zao kuendelea. Tuwatetee.
Amemshukuru Mungu Kwa kumpa Mke jasiri anayempa moyo na Ndio ngome yake Kwa sasa.

Nimemwomba Lema aone kuwa hii struggle sio yake peke yake bali anawakilisha watu wengi wanaotaka Haki kutendeka Katika uendeshaji wa Nchi yetu. Siku zote Haki hushinda''
BREAKING NEWS: ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA GEREZANI KISONGO ASEMA LEMA ANA ARI YA MAPAMBANO BREAKING NEWS: ZITTO KABWE AMTEMBELEA LEMA GEREZANI KISONGO ASEMA LEMA ANA ARI YA MAPAMBANO Reviewed by WANGOFIRA on 08:52:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.