Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro, amesema kama Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, ana wasiwasi na Jeshi la Polisi katika operesheni ya kutokomeza matumizi ya Shisha, achukue hatua zaidi kwa sababu yeye ni kiongozi wao na ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani Dar es salaam.

Akiongea kupitia kipindi cha Sun Rise cha Times Fm leo asubuhi, Sirro amedai wao kama jeshi la Polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho baki ni Mwanasheria mkuu wa Serikali kuandaa mashtaka kwa Watuhumiwa.

“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasi wasi kama wasi wasi basi unabaki kuwa wasi wasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni, yeye ni mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya.

“Lakini kama ana wasi wasi Zaidi yeye ni kiongozi wetu atajua atachukua hatua gani dhidi ya sisi, kwa hiyo namuachia mkuu wangu wa kazi yeye ndio atajua nini cha kufanya”

Akitolea ufafanuzi kama alipatiwa taarifa juu ya watu 10 waliotaka kumpa ‘Mlungula’ Mkuu wa Mkoa ili kumziba ‘Mdomo’ kukemea matumizi ya kilevi cha Shisha, Kamanda Siro alisema hawezi kulisemea lolote swala hilo na amemtaka Mtangazaji wa Sun Rise Stanslaus Lambat amuulize Mh Makonda taarifa aliipeleka wapi na si yeye.
Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu Kamanda Sirro: Makonda ni Mwenyekiti wangu, Kama ana wasiwasi Atajua atachukua hatua gani dhidi yetu Reviewed by Unknown on 05:51:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.