Benki ya AMANA yazindua Huduma ya Mikopo midogo midogo kwa wafanya Biashara Mbagala Jijini Dar es Salaam
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es
salaam Mh Abdala Mtimika (Kushoto) Pamoja na Mkurugenzi wa Bank ya
Amana nchini Dr Mosen Masoud wakikata utepe Kuashiria kuzinduliwa Rasmi kwa
Huduma ya mikopo Midogo Midogo kwa wafanya biashara wa Mbagala Jijini Dar es
salaam.uzinduzi huo umefanyika katika Tawi la Amana Mbagala(Picha zote na Vicent Macha wa Habari24 blog)
|
Hatimaye wakazi wa mbagala
wanaofanya Biashara ndogo ndogo wakiwemo wajasiriamali wamepata neema kubwa
baada ya Bank ya AMANA kuzinduaa huduma yake mpya ya kutoa mikopo midogo midogo
kwa wafanya biashara, huduma ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es salaam ikiwa
ni miaka mitano Tangu kuanzishwa kwa Bank Hiyo.
Akizungumza na wanahabari na wananchi wa
mbagala ambapo ndio uzinduzi huo umefanyika Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen
Masoud amesema kuwa huduma hiyo imeanzishwa mahususi kwa kutambua hitajio kubwa
katika jamii la wafanya biashara wadogo wadogo katika kupata mtaji ya kukuza
biashara zao hivyo Bank ya Amana imeamua kuwainua wafanya biashara hao wadogo
ili kuinuka kipato chao na kufikia kipato cha kati na hata kipato cha juu.
Amesema kuwa kupitia huduma hiyo Amana
Bank inawawezesha wafanya biashara kwa kununua bidhaa wanazohitaji katika
biashara zao na kuwauzia kwa bei nafuu kwa mkopo ambapo watarejesha kidogo
kidogo katika muda ambao umewekwa katika utaratibu.
Mkurugenzi wa Bank Hiyo Dr Mosen Masoud akizungumza
na wanahabari na wananchi waliofika katika uzinduzi huo
|
Ameongeza kuwa wafanyabiashara sasa wana
nafasi ya kukodishwa vifaa mbalimbali wanavyohitaji katika kuendesha biashara
zao kwa kodi nafuu na mwishowe wanaweza wakanunua vifaa hivyo kwa Bei nafuu
Mkurugenzi huyo ameendelea kueleza kuwa
kwa sasa Huduma hiyo ya mkopo imeanza kutolewa kwa wateja wake wanaotumia Tawi
lao la Mbagala tu lakini kusudi lao ni kuhakikisha kuwa wanaendesha zoezi hiyo
latika matawi yao yote nchini ambayo kwa sasa yapo matawi saba.
Diwani wa Kata ya kibonde Maji mbagala Jijini Dar es
salaam Mh Abdala Mtimika Akizungumza
|
Akizunguza wakati wa uzinduzi huo Mgeni
Rasmi ambaye ni Diwani wa kata ya Kibondemaji Abdala Mtimika ambaye
alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Temeke amesema kuwa Uzinduzi wa Huduma hiyo ya
kutoa mikopo midogo modogo sasa imekuja wakati muafaka kipindi ambacho
watanzania wengi wamekuwa wakilalamika kudorora kwa uchumi na pesa kupotea
hivyo ni jukumu la wafanya biashara wa mbagala kutumia nafasi hiyo adhimi
kuhakikisha kuwa wanapata mikopo hiyo na kuwekeza katika Biashara zao.
Wiki ya Huduma kwa wateja ikiendelea wateja
mbalimbali wakipata Huduma katika Tawi la Benk hiyo Mbagala leo
|
Aidha Diwani huyo amewapongeza sana
uongozi wa Bank ya Amana Tanzania kwa kuweza kuendesha Bank hiyo kwa usawa
pamoja na kuwa imekuwa ikijulikana kuwa Ni Bank ya kiislam ila sio kweli kwani
imekuwa ikitoa Huduma kwa watanzania wote bila kujali Dini zao pamoja na kuwa
inatumia Taratibu za kiislam.
Wanahabari wakiwa katika hafla hiyo
|
Uzinduzi wa huduma hiyo umekwenda sambamba
na uzinduzi wa wiki ya Huduma kwa mteja ambapo bank hiyo imeanza kuadhimisha
wiki hiyo leo ikiwa ni kuendelea kusherekea miaka Mitano ya Bank hiyo tangu
ianze kutoa huduma za kibenk nchini Tanzania.
Benki ya AMANA yazindua Huduma ya Mikopo midogo midogo kwa wafanya Biashara Mbagala Jijini Dar es Salaam
Reviewed by WANGOFIRA
on
19:55:00
Rating:
No comments: