Umoja wa Mataifa kuimarisha kikosi chake cha kusimamia amani CAR



Mkurugenzi wa Masuala ya Mawasiliano ya Wasimamia Amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ametangaza kuwa, umoja huo una mpango wa kuimarisha zaidi kikosi chake katika nchi hiyo.

Hervé Verhoosel ameeleza kuwa, Umoja wa Mataifa umeazimia kuongeza idadi ya askari wake wa kusimamia amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Verhoosel ameelezea kuwa, shughuli ya kusimamia amani ya kikosi hicho kinachojulikana kama MINUSCA zitapanuka katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa unatangaza uamuzi wake wa kupanua shughuli za kikosi chake cha kusimamia amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika hali ambayo, huko nyuma askari wake wamewahi kukabiliwa na tuhuma nyingi za vitendo vya kubaka na kunajisi.

Kikosi cha kulinda amani chah UN nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA)


Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika machafuko na mapigano tangu mwaka 2013 wakati makundi ya Kikristo yanayobeba silaha yalipoanzisha mashambulio yaliyoratibiwa dhidi ya kundi la Seleka lenye Waislamu wengi zaidi, ambalo mnamo mwezi Machi mwaka huo liliiondoa madarakani serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Francois Bozize.

Kufuatia machafuko hayo raia wengi wameyakimbia makazi yao na kuishi maisha ya ukimbizi ndani na nje ya nchi hiyo. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, karibu raia laki nne wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakimbizi huku kumi na moja elfu kati yao wakiomba hifadhi katika nchi jirani.

Chanzo: parstoday.com
Umoja wa Mataifa kuimarisha kikosi chake cha kusimamia amani CAR Umoja wa Mataifa kuimarisha kikosi chake cha kusimamia amani CAR Reviewed by WANGOFIRA on 20:46:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.