SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTANZIR YA JIJINI DAR ES SALAAM YATOZWA FAINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA


Shule ya sekondari ya Almuntazir iliyopo upanga jijini Dae es salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini zinazotakiwa kisheria.

Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina iliyofuatia malalamiko ya wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri kufanya ziara yakwenda kujionea uchafuzi huo.

Akiongea kwa Niaba ya shule meneja wa shule hiyo Bw. Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea swala la ukuta wa shule hiyo.

Naibu Waziri Mpina amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekeajia wakiukaji wa sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.

Aidha Naibu Waziri alitembelea maeneo  ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa mazingira uliotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo ya mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa ya maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.

Akiikemea DAWASCO kwa mara nyingine kwa kutokuonyesha uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu, Naibu Waziri Mpina ameita NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.

Na, EVELYN MKOKOI
DAR ES SALAAM
27/10/2016



SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTANZIR YA JIJINI DAR ES SALAAM YATOZWA FAINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTANZIR YA JIJINI DAR ES SALAAM YATOZWA FAINI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA Reviewed by WANGOFIRA on 14:21:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.