Serikali Yaiamuru Bodi ya Mikopo Istishe Makato na Imlipe Pesa Zake Mstaafu Aliyekuwa Akikatwa Kimakosa

Serikali  imeiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kusitisha mara moja makato ya fedha yaliyokuwa yakifanywa kwenye malipo ya pensheni ya mstaafu Ernest Lameck, katika Chuo cha Ualimu cha Tukuyu kilichopo wilayani Rungwe.

Agizo la kusitishwa kwa makato hayo limetolewa baada ya kubainika kuwa deni hilo ni hewa kwa kuwa mtumishi huyo mstaafu hakuwahi kusoma katika chuo cha Elimu ya Juu.

Amesema Bodi ya Mikopo imekuwa ikitoa mikopo na kwamba kinachofanywa na taasisi hiyo ya Serikali ni wizi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara katika Chuo cha Ualimu Tukuyu na kuelezwa juu ya uwepo wa mstaafu huyo ambaye amekuwa akikatwa fedha wakati si mnufaika wa mkopo.

Mkuu wa chuo hicho, Ubaya Salumu, amemweleza Waziri kuwa Lameck aliyekuwa mtumishi chuoni hapo alianza kukatwa fedha kwenye pensheni yake na alipofuatilia alibaini kuwa makato yamekuwa yakifanywa na Bodi ya Mikopo.

Amesema jambo la kushangaza ni kuwa kabla na wakati wa utumishi wake, Lameck hakuwahi kusoma elimu ya juu ambayo angeweza kuomba mkopo kutoka katika bodi hiyo.

Lameck amebainisha kuwa baada ya kufuatilia alibaini kuwa Bodi ya Mikopo inamdai Sh milioni tisa na ni kwa muda mrefu amejaribu kufuatilia jambo hilo pasipo mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Ndalichako mbali na kuiagiza bodi kusitisha makato hayo mara moja, pia aliagiza fedha zote alizokatwa mtumishi huyo zirejeshwe ili anufaike na stahili zake.

“Haiwezekani mtu haukukopeshwa halafu waanze kumkata. Hili nataka lifanyike haraka na si tu kusitisha makato, bali lazima Bodi wakulipe fedha zako zote walizokukata,” alisisitiza.
Serikali Yaiamuru Bodi ya Mikopo Istishe Makato na Imlipe Pesa Zake Mstaafu Aliyekuwa Akikatwa Kimakosa Serikali Yaiamuru Bodi ya Mikopo Istishe Makato na Imlipe Pesa Zake Mstaafu Aliyekuwa Akikatwa Kimakosa Reviewed by WANGOFIRA on 01:15:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.