JWTZ WAWASILI KAGERA KUJENGA MIUNDO MBINU YA SERIKALI ILIYOHARIBIWA VIBAYA NA TETEMEKO LA ARDHI


Kikosi kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao makuu ya Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya serikali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoana Kagera septemba 10 mwaka huu. 


Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho kinawataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya ujenzi. 


"Hiki kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku na mchana taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni pamoja na mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa waendelee kupata matibabu"alisema. 


Alisema mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa umekamilika kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano maeneo yote watakayopita kujenga miundombinu ya umma. 


Kiongozi wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi hicho kimekuja Kagera kusaidia serekali ya Mkoa kurudisha miundombinu yote ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya kawaida. 


"Ni vigumu kusema lini tutakamilisha ujenzi ila sisi tutafanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huu ukamilike ndani ya muda mfupi"Alisema Meja Kakura. 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi 
JWTZ WAWASILI KAGERA KUJENGA MIUNDO MBINU YA SERIKALI ILIYOHARIBIWA VIBAYA NA TETEMEKO LA ARDHI JWTZ WAWASILI KAGERA KUJENGA MIUNDO MBINU YA SERIKALI ILIYOHARIBIWA VIBAYA NA TETEMEKO LA ARDHI Reviewed by WANGOFIRA on 01:23:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.