JAMAA AJICHINJA BAADA YA MPENZI WAKE KUCHUKULIWA NA MWANAMME MWINGINE DODOMA


Mwanamme aliyejichinja shingo akisaidiwa na wasamaria wema-Picha na Andrew Msafiri
 ******
 Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamme mmoja ambaye hajajulikana jina anayedaiwa kuwa ni mfanya biashara katika stendi ya mabasi ya Mpwapwa mkoani Dodoma amejichinja kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tukio hilo  limetokea leo Oktoba 25,2016 majira ya saa sita mchana baada ya jamaa huyo kukataliwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.

“Amejikata koromeo kwa kutumia kisu baada ya mwanamke aliyekuwa naye kumkataa kwa madai kuwa ana mwanamme mwingine,kitendo cha mpenzi wake kuchukuliwa na mwanamme mwingine ndicho kimemfanya achukue maamuzi hayo magumu ya kuondoa uhai wake”,
Inaelezwa kuwa mwanamke huyo pamoja na mwanamme anayedaiwa kuchukua mpenzi wa mwanamme aliyejichinja pia wanafanya kazi katika stand hiyo ya mabasi.

Hata hivyo kutokana na kitendo hicho wasamaria walijitokeza kumsaidia mwanamme huyo na kumkimbiza katika hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya matibabu. 

Na Andrew Msafiri
JAMAA AJICHINJA BAADA YA MPENZI WAKE KUCHUKULIWA NA MWANAMME MWINGINE DODOMA JAMAA AJICHINJA BAADA YA MPENZI WAKE KUCHUKULIWA NA MWANAMME MWINGINE DODOMA Reviewed by WANGOFIRA on 20:52:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.