SHIME ATAJA KILICHOISIBU SERENGETI KURUHUSU MAGOLI NYUMBANI

img_3864
Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime amesema, kuwakosa wachezaji wake wawili kwenye kikosi cha kwanza kumechangia timu yake kuruhusu magoli mawili kwenyeuwanja wa nyumbani dhidi ya Congo Brazzaville wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa timu za vijana (U17) zitakazofanyika Madagascar mwaka 2017.
Shime amemtaja beki wa kati Dickson Job pamoja na kiungo Ally Nyanzi kuwa kukosekana kwao kulikuwa ni pengo ambalo madhara yake ni kuruhusu magoli mawili kwenye uwanja wa nyumbani.
“Mapungufu ya kumkosa beki wetu wa kati Dickson Job na kiungo Ally Nyanzi yameathiri timu yetu lakini katika mchezo wa marudiano watakuwepo uwanjani na timu yetu itakuwa strong zaidi”, alisema Shime mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Serengeti Boys huku timu yake ikishinda kwa magoli 3-2.
Shime alipoulizwa kama timu yake itaweza kufuzu kutokana na kuruhusu magoli mawili nyumbani ambayo yatawapa kazi ngumu kwenye mechi ya marudiano alisema, kama Congo wameweza kufunga hapa basi hata Serengeti inaweza kupata magoli ugenini.
“Hakuna ushindi mdogo kwenye mchezo wa soka, kama wao wameweza kufunga magoli, sisi vilevile tunaweza kufunga magoli ugenini. Timu yangu imekuwa na rekodi ya kufunga magoli kwenye viwanja vyovyote vile, tumeweza kufunga magoli kwenye viwanja vya ugenini na nyumbani.”
“Siogopi, tutaweza kulinda vizuri ugenini na kushinda. Katika mechi nane, tumefungwa magoli mawili ya penati na moja la kawaida, kwahiyo unaweza kuona tuna safu nzuri ya ulinzi kwa kiasi gani.”
“Walionekana kutuzidi nguvu lakini nimeelezea kwamba timu yetu ilikuwa na mapungufu kidogo katika sehemu ya ulinzi kwahiyo timu yangu haikuwa kwenye ubora wa kila wakati.”
“Timu bora inashinda popote pale Serengeti ni timu bora, imeshinda mechi zote za nyumbani na haijafungwa mechi hata moja ugenini. Bado tunanafasi ya kushinda Congo au kutoka sare.”

Source: Shaffih DaudaRead More 
SHIME ATAJA KILICHOISIBU SERENGETI KURUHUSU MAGOLI NYUMBANI SHIME ATAJA KILICHOISIBU SERENGETI KURUHUSU MAGOLI NYUMBANI Reviewed by WANGOFIRA on 19:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.