RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 37 & 38 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
    
Ilipoishia...
Roho ya huruma ikaniingia na kujikuta nikianza kukimbia na kuwakumba watu waliopo mbele yangu na kujikuta nikisimama gafla huku macho ni kiwa nimeyatoa kiasi kwamba hasira ikazi kunipanda hii ni baada ya kumkuta ni mama yangu ndio anaye pigwa na askari hawa wanao onekana hawana huruma kabiasa wa watumwa walipo ndani ya hili pango.

Endelea....
Nikajirusha juu ya mwili wa mama yangua na kumkumbatia kitendo kilicho zidisha hasira ya askari hawa na wakaanza kunishambulia mimi kwa kunipiga,sikaanza kusikia uzito mwengine ukija juu yangu na nikagundua kuwa watumwa wengine wamepatawa na roho ya huruma na wao mwaneamua kufanya kama nilivyo fanya mimi na kwa umoja wetu ikawalazimu askari kusitisha zoezi lao la kutupiga.

Wakatuamuru tuweze kurudi kwenye kazi za kuvunja miamba,nikamnyanyua mama taratibu huku uso wake ukiwa umejawa na damu zilizo changanyikana na machozi mengi.Nikamshika mama huku akiwa hatambui ni nani aliye mshika na kabla sijamsemesha kitu cha ina yoyote askari mmoja anisukuma ili nimuechie mama kisha akamshika mama mkono na kuanza kumburuza kitendo kilicho zidi  kunipandisha hasira ila kabla sijhamfwata nikastukia nikichapwa na fimbo aina ya mkia wa taa iliyo jizungusha kwenye tumbo langu na kunirudisha nyuma baada ya askari aliye nichapa kafanya hivyo bila ya huruma.

Nikamshuhudia mama akipotelea gizani kwenye pango pamoja na askari aliye mchukua na sikuwa na lakufanya zaidi ya kuendelea kupokea kichapo cha kuchapwa nikiamrishwa kwenda kufanya kazi upasuaji wa mame.Nikaokota moja ya nyundo huku nikiwa na hasira na uchungu mwingi na kuaza kuvunja mwamba amabao wenzangu wanaendelea kuuvunja.Kitu ambacho nimegundua ni kwamba watu wengi waliomo humu ndani wamelishwa makaa ya mawe moto ambaya sio rahisi kwa mtu kuweza kuzungumza chocheta zaidi ya kutoa miguno.

Hali ya maisha ikazidi kuwa ngumu kwa upande wangu kadri ya siku zinavyo zidi kwenda sikuweza kumuona mama yangu japo ninaendelea kufanya juhudi ya kuchunguza ni wapi alipo mama na sikuwa ninafahamu kama yupo hai au tayari amesha fariki,mwili wangu ukazidi kudhohofika kutokana na chakula finyu tunacho pewa asubuhi na jiono,asabuhi tunakunywa kikombe kidogo cha uji usio na kadha ya aina yoyote na usiku tunapewa viazi viwili vilivyo chemshwa na huo ndio mlo wa siku moja na mbaya zaidi chakula ni chakugombani usipo fanya hivyo unaweza kukaa siku mbili hadi tatu pasipo kula.

Watu wengi wanazidi kufa kutokana na njaa inayo andamana na kazi ngumu kwa upande wangu kifua kianza kuniuma sana ikafikia hatua nikaanza kukohoa na makohozi yangu yamechanganyikana na damu nyingi.

“hapana siwezi kufa humu ndani”
Nimawazo ambayo yakawa yanajirudia rudia kichwani kwangu kadri siku zinavyo zidi kwenda,mbaya zaidi sikuweza kujua upi ni usiku na upi ni mchana hii ni kutokana na muda wote tuliopo ndani ya pango mataa makubwa yanawaka,kila ninapo jitazama mwili wangu ninajikuta nikimwagikwa na machozi kwani mbavu zangu unaweza kuzihesabu,mikono na miguu yangu imekondeana sana.Nyele zangu zimekosa uhusiano mzuri kichwani vidonda vingi ambavyi vingine vimefikia hadi hatua ya kutoka na funza vikaendelea kunitesa mwili wangu.

“mungu wangu ninaomba unipe nguvu na juhudi katika hili”
Nikaanza kufanya kazi ya kutafuta ni wapi ninaweza kupata njia ya kutokea na kwa bahati nzuri katika uvunjaji wangu wa miamba nikaona sehemu yenye ufana wenye kijisihimo kidogo,nikawatazama askari waliopo ndani humu na hakuna aliye nifwatiliza nikapiga hatua za taratibu na kuchungulia kwenye shimo na kuona mwanga kwa mbali na akili yangu ikatambua utakuwa ni mwanga wa jua.

Kengele ya kwenda kupata chakula cha jioni ikagongwa na nikatupa sururu niliyo nayo chini na kuchomoja kwa kasi kuwania chakula ambacho nikikosa leo itakuwa siku yangu ya pili kukosa chakula.Japo mwili wangu umedhohofika nikajikaza katika kugombani viazi na kupata viazi vitatu,nikakaa kwenye sehemu ambayo siku zote huwa  ninapenda kukaa na kuanza kuvisakamia viazi kwa fujo

Nikastukia nikiguswa mguu na binti mdogo na akaniwekea mkono kwa ishara ya kuniomba kiazi kimoja ambacho nimebaki nacho mkononi.Nikamtazama kwa jinsi alivyo kondeana hadi sura yake imejaa vishimo shimo vilivyo kosa nyma kwa kukondeana.Taratibu nikampa kijikiazi nilicho nacho na chote akakiweka mdomoni na kuanza kukitafuna kwa haraka na inavyo onyesha ana njaa kuliko mimi.Akanishukuru kwa kuikutanisha mikono yake kwa pamoja huku akiinama na akanyanyuka taratibu na kuondoka.

Tukuruhusiwa kwenda kulala kwenye mapango yetu ambayo milango yake ni ya chuma na katika chumba kimoja cha pango tunalala watu si chini ya thelathini na tangu niingie kwenye hili pango sikuwahi kuona hata siku moja watu wakienda kuoga kwahi maji tunayo kunywa ni machafu sana na yapo kwenye kijikisima kimoja kidogo.Harufu ya uchafu wa miili yetu siku zote inanikusesha raha ya kulala na hususani loe kidogo ninajambo la kuliwazia kichwani kwangu kutokana na ufana nilio uona ninaimani utanisaidia katika kutoroka ndani ya hili pango.

Muda wa kuamshwa ukawadia na tukatoka ndani ya vyomba vyetu na kuelekea sehemu za utendaji wetu wa kazi na kitu cha kwanza kufika kwenye sehemu yangu nikawa na kazi ya kuvujunya ufa nilio uona,ugumu wa mwamba huu hakunifanya nife moyo zaidi ya nilicho kifanya ni kuendelea kuvunja hadi ikafikia kipindi matumaini yakaaza kuja,filimbi ya dharura ikapangwa na tukakusanyika kwenye eneo la moja na askari wakaanza kutupanga mistari mitatu na tukasubiria nini tunacho taka kuambiwa.

Nikawaona watu wanne walio valia vizuri na nikamgundua mmoja wao ambaye ni baba yangu mkubwa mzee godwin akiwa ameongozana na watu wengine watatu ambao sikuwajua.Mukuu wa askari wa eneo hili akawapokea kwa unyeyekevu mkubwa na kuanza kuwapitisha kwa kwenye mistari mmoja baada ya mwengine kama vile raisi anaye kagua gwaride la wanajeshi.
  
Sura yangu nikaiinamisha chini ili asiweze kunijua kwa haraka na kabla ya kunifikia mimi akahamia kwenye mstari wa nyuma yetu na kuendelea kuwatazama watumwa wezangu tuliopo kwenye eneo hili,wakamaliza kazi hii na wakapanda kwenye ofisi ya mkuu wa eneo hili huku wakizungumza na kucheka kwa furaha.

Uchungu na maumivu makali yakaendelea kuutesa moyo wangu ila sikuwa jinsi,tukarudi kwenye sehemu zetu na kuendelea na kazi hata kengele ya uji ilivyo gonga sikuwa na haja ya kwenda kugombania uji.Nikaendelea kupasua mwamba huu na kugundua mawe haya nikiyagonganisha kwa pamoja yanaweza yakazalisha moto kutokana na chechezake.Nikawaona askari wanao tusimamia wakielekea walipo kwenda baba na wezake wakionekana kujawa na furaha hapa ndipo nikaamini kuwa baba mkubwa ndio mmiliki wa hili eneo.

Kwa bahati nzuri nikaona kamba moja ambayo hutumia katika kubutia mawe makubwa,nikaichukua na kwenda moja kwa moja kwenye mapipa yenye mafuta ya petrol ambayo yanatumika kuendeshea majenereta yanayo washa taa za humu ndani,kwa haraka nikaichovya kamba kwenye pipa lenye mafuta na kabla sijaondoka eneo lenye mapipa nikaona kidungu kidogo cha maji ya lita moja na nusu.

Nikakiokota na kuchota mafuta nusu na kurudi katika eneo lenye ufa,kwa uzuri ni kwaba sehemu yenye ufa juu yake ndipo zilipo ofisi za wakuu wa hii sehemu na haikuw ni raisi kwa wao kuniona kutokana nipo chini shana na pameingia ndani.Wezangu tayari wamesha toka kunywa uji na wanaendelea na kazi zao za upasuaji wa mawe na kelele za upasuaji wa mawe zikazidi kunipa moyo wa kwamba sio rahisi kwa maaskari kuweza kusikia kitu cha aina yoyote.

Nikaiingiza kamba kwenye mdomo wa kidungu nilicho kiokota japo kamba ni nene kiasi ila nikajitahidi kuigandamiza hivyo hivyo na ikaingia kiasi kidogo.Nikakichomeka kidungu sehemu yenye ufa na kabla sija ondoka kwenye eneo hili msichana aliye niomba kiazi jana usiku akanifwata na kunigusa mkono na kwa ishara akaanza kunielekeza kitu ambacho haikuwa si raisi kwa mimi kuielewa

Nikaivuta kamba yangu hadi sehemu yenye umbali kidogo na eneo lenye ufa na kuokota mawe mwili ya mwamba na kuanza kuyagonganisha kwa nguvu.Kila ninavyo endelea kuyagonganisha ndivyo jinsi msichana anavyo nisumbua kwa kunishika mkono na kunionyesha kwa ishara umbo la binadamu na kudai kuwa lipo kwenye sehemu ya pili ya sehemu ninayo ipasua.

Japo ninamuelewa ila sikuwa na haja ya kusikiliza sana na nikazidi kujitahidi kuyagonganisha mawe yangu kwa nguvu na kasi ya kubwa hadi chche zikaanza kutoka na kwabahati nzuri cheche baadhi zikanasa kwenye kamba yenye mafuta ya petrol na kwa kasi ikaanza kuwaka huku ikielekea sehemu yenye kidungu cha maputa.Msichana anakigeuza ili nisome kitu alicho kiandika sehemu ya ukutani kwenye mwamba kwa kutimia jiwe.Nikakutana na maandishi yenye herufi kubwa na zilizo kaa bila mpangilio zinazosomeka.

{mama uliye mtetea siku zileeee yupo sehemu ya pili ya sehemu ambayo unapasua huo mwamb…..}.Kabla sijamalizia kusoma maandishi hayo nikastukia mlipuko mkubwa ulio sababisha mwamba kupasuka na kuanza kudondosha mawe makubwa ambayo yameanza kuwaangukia watumwa wezangu pamoja na kuta za ofisi zilizopo juu kuanza kumeguka taratibu na kuporomoka chini

                           *****sory madam*****(38)

Mawe yakazidi kuporomoka huku vilio na kelele zikitawala kwenye pango zima,binti niliye naye akanishika mkono na kuniomba nimfwate huku tukijaribu kuyakwepa mawe yanayo endelea kuanguaka,tukafanikiwa kufika kwenye moja ya kijiuchochoro na tukapita na kutokea kwenye moja ya kijimlango cha mbao na akaniomba nichungulie ndani kupitia nondo mbili zilizopo kwenye mlango.

Nikamuona mama akiwa amelala chini huku panya na wadudu wengi wakiwa wanamtambalia,hali yake imedhoohofika sana mimi kidogo ninanafuu.Nikatafuta kipande cha jiwe kikubwa na kuanza kupiga kwenye mlango huu ambao ni wa mbao.Nikaendelea kusaidiana na binti niliye kuwa naye na tukafani kiwa kuipasua mbao moja ya mlango,kutokana na wembamba wangu nikafanikiwa kupennya ndani na kumkuta mama akikoroma sana akiwa anaelekea kwenye hatua za mwisho mwisho za maisha.

“mama…..Mama mama”
Nimuita mama na akayafumua macho yake taratibu na kunitazama na hakuamini kama ni mimi ndio ninaye muita,akaachia tabasamu pana nikamnyanyua na kuanza kumpitisha kwenye kijiuwazi japo ni kwashida sana ila ikanilazimu kufanya hivyo.

Tetemeko la ardhi likaanza kutikisika na woga ukazidi kunitawala,nikafanikikiwa kimtoa mama kwenye kijiupenyo cha mlango kisha na mimi nikaanza kupenya ila kabla sikamalizia kutoka nikajikita nikipiga kelele ya uchungu hii ni kutokana na jiwe lenye ncha kali kutua juu ya mguu wangu wa kushoto.Mama na msichana mdogo wakaanza kunivuta nje japo kwa mama kidogo hakuwa na nguvu sana.

Nikatoka nje ya kijishimo na kuutazama vizuri mguu wangu na kuundua kuwa umetobolewa vibaya maeneo ya kigimbi na kipande kidogo cha jiwe kimekatikia ndani ya mguu.Kila nilipo jaribu kunyanyuka nikajikiya nikishinda na kukaa chini.Tetemeko kubwa la ardhi likaendelea kutetemesha kila eneo na mawe yakazidi kuanguka
“e…ddy…mwan…gu jiiikazeee”

Maneno ya mama yakanipa matumaini mapya ya kujiokoa,nikasimama wima huku meno yangu nikiwa nimeyang’ata nikisikilizi maumivu jinsi yanavyo vuta kwenye mguu wangu.Tukaanza kusikia mlio mkubwa wa maji na gafla tukastukia maji mengi yakija nyuma yetu kwa kasi kubwa na moja kwa moja nikatambua kuwa sehemu ambayo tupo kuna mwamba wa maji umepasuka.Mama akanikumbatia kwa nguvu na binti mdogo niliye kuwa naye ananing’ang’ania mkono na sote maji yakatunyanyua na tukaungana na watu wengi waliobebwa kwenye maji haya.

Ikawa ni kazi ya kumuomba mungu tunapo elekea tusikutane na kitu ambacho kitaweza kutudhuru.Mama wala binti mdogo hakuna aliye niachia na kila mmoja akajitahidi kwa uwezo weke kunishikilia kwa nguvu zake zote.Ikawa ni kazi yangu kujitahidi kupata muhumili wa kuendana na maji haya kwani watu wengine waliojiachia walijikuta wakikigonga vichwa kwenye mawe ambayao yanaendelea kupasuka na ikawa ni safari ya maisha yao japo miili yao iliendelea kuendelea kupelekwa na maji kama tunavyo pelekwa sisi.

Maji yakazidi kutupekeka kwa kasi cha kumshukuru mungu nikafanikiwa kushika maja ya jiwe lililo simama kama nguzo,kila nilipo mtaza mama usoni nikajikuta nikipata moyo wa kuuendelea kumsaidia mama kwa moyo mmoja na wakaendelea kunishikilia japo ninapata maumivu kwenye viganja vyangu ambaco hadi kwa sasa vimeota sugu kutokana na upasuaji wa mawe ila nikajikaza kama mwanaume.
“bora nife mimi ila si mama yangu”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijitahidi kuikanza mikono yangu ili maji yasizidi kutupeleka mbele zaidi,kwa bahati mbaya mwili wa mtu ukaja kutua kwenye jiwe nililo lishikikilia na kuvigandamiza viganja vyangu kwa nguvu hadi nikajihisi vidole vinaweza kukatika na taratibu nikajikuta nikachina na safari ya maji ikaanza kutupeleka huku tukiwa tumetanguliza miguu.

Nikaanza kuona mwanga kwa mbali kidogo ambapo ndipo maji yanapo tokea.Wasiwasi mwingi ukaanza kuniingia na nikiwa katikati ya mawazo hayo nikastukia tukuchomolewa ndani ya pango na kuanza kwenda chini ambapo ndipo maji yanapo elekea.Nikagundua sehemu tunayo kwenda kuangukia ni kwenye bahari.

Sote tukaingia ndani ya bahari na kushuka chini kidogo na nikajihisi wepesi na nikaanza kuogelea kurudi juu,hadi ninatokeza kwenye usawa wa bahari nikajikuta nipo peke yangu sikumuona mama wala msichana mdogo.Baridi kali ikazidi kunitesa na mbaya zaidi sehemu kubwa ya bahari imezungukwa na milima mingi.

Nikavuta pumzi nyingi ya kutosha na kurudi ndani ya maji na kuangaza kila sehemu ila sikuweza kumuona mama wala masichana mdogo.Nikarudi tena juu na kumuona msichana mdogo akinywa maji kwa mkupuo,kwa haraka nikaanza kuogelea hadi sehemu alipo na nikamuacha kudogo nguvu zimuishie ndipo nikaipitisha mikono yangu chini na kuushika mgongo wake ili aelele juu kidogo na macho yangu yakawa na kazi ya kutazama ni wapi alipo mama.

Nikamuona mama akiibuka kwenye maji kwa mbali kidogo na kutokana na kuchoka sana sikuwa na hata na uwezo wa kumuita kwa sauti yajuu.Mama akaanza kupiga mbizi taratibi hadi nillipo mimi na akanisaidia kuipitisha mikono yake chini na ikakutana na mikono yangu kwa chini na tukashikana tukiwa hatujua nini cha kufanya kwa maana sehemu tuliyopo ni mbali sana kinho za bahari.

Jua likaanza kuzama taratibu huku baridi ikizidi kuongezeka na kwabahati nzuri tukaona boti ndogo inayo kwenda kwa kasi ikipita maeneo ya karibu nasi.Kwa hungu nikapiga kelele za kuomba msaada huku nikisaidiana na mama,ikatupita na kujikuta tukinyamaza tukiiangalia jinsi inavyo tokomea kwenye maji na matumaini ya kuokolewa ikakata
“kama mungu aliye tusaidia tukatoka pangoni na kutufikisha hapa ninaimani yeye pia atatusaidia kupata msaada”

Mama alizungumza huku akiutasama usawa wa biti ilipo elekea kisha akanigeukia na mimi huku machi yakianza kumlenga lenga.Unene wa kiasi wa mama yangu umepota wote,uzuri na taswira yake ya kuvutia imepotea na sura yake imeingia uzee wa gafla huku akiwa amekondeana sana.

“haki ya mungu nikirudi hai lazima nilipize kisasi kwa mzee godwin”
Nilijiapiza kimoyo moyo huku nikimuangalia mama kwa huruma sana,msichana mdogo hali yake ikaanza kuwa mbaya.Mwili wake ulianza kutetemeka huku kmapovu mengi yakimwagika mdomoni
“mama ana nini huyu”

“ni kifafa hambe jikaze kidogo mikono yako mimi ninaachia”
Nikafanya kama mama anavyo nihitaji na nikaikaza mikono yangu na mama akaitoa mikono yake na kuushika mdomo ya mtoto  mdogo na kuanza kuziachanisha taya zake ili asiung’ate ulimi wake,gafla kwa mbali sana nikaanza kuona kitu kikija kwa kasi huku kikiwa kimejitokeza upanga mmoja na kwaharaka nikatambua ni papa.

“ma…”
“nini?”
“ona huko nyuma”
Mama akatizama nyuma na nikastukia akiacha alichokuwa akikifanya kwa msichana na kwa haraka akaniomba niogelee na nimuache msicha.
“mama”
“fanya kama nilivyo kuambia okoa maisha yako kwanza huyo binti muache”

Mama alizungumza huku akiendelea kupiga mbizi akielekea upande mwengine,roho ya huruma ikanijaa moyoni mwangu na ninakafikiria mambo machache aliyo nifanyia huyu binti kwani isinge kuwa ni yeye nisingeweza kumuona mama na kwa haraka nikamuweka mgongoni kisha nikaivua suruali yangu iliyo chakaa na kubakiwa kama nilivyo zaliwa na kumfunga vizuri ili asianguke na kuanza kuogelea kuelekea kwa haraka alipo mama.

Japo kuna uzito ila nikaendelea kujikaza kama mwanaume.Na jinsi ninavyo ogelea kwenda mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo

  Itaendelea...
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 37 & 38 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 37 & 38 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 21:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.