RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 35 & 36 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )


Mtunzi:EDDAZARIA G.MSULWA
 
Ilipoishia...

Daktari aliye kuwa anaendelea kunipiga baada ya kumuona mwenzake akiwa anaaga dunia akaniacha na kwa nguvu zake zote akarusha kirungu chake na kikatua kichwani mwa sheila na akadondoka chini na damu za puani zikaanza kumwagika

Endelea....

Taratiu nikaanza kujiburuza chini hadi sehemu aliyo angukia sheila huku machozi yakinimwagika na kujikuta nikijilaza juu yake na kumfanya daktari aliye mpiga akanza kunipiga tena kwenye mgongo akinimrisha nimuechie sheila ili aendelea kumshuhulikia kwa kipigo.Kila nilipo jaribu kumtingisha sheila sikuweza kuona dalili yoyote ya kuishi kwake na kujikuta nikizidi kumkumbatia kwa uchungu.Nikaanza kusikia makelele yakija kwa nyuma yangu,nikageuza shingo yangu na kuona kundi kubwa la vichaa wakija kwa kasi na kumfanya daktari anaye nipiga kutimka mbio na sikujua ni wapi anapo elekea na wote wakanipita na kuendeleka kumkimbiza dakrari aliye kuwa akinipiga.
 
Nikaona nikiendelea kujiliza haita saidi zaidi ya kumfanya sheila kuzidi kuzidiwa na kipigo alicho kipata.Nikajikaza na kwabahati nzuri miguu yangu ina nguvu za kutosha nikanyanyuka na kujinyoosha japo nilijawa na maumivu makali ila sikuwa na jinsi.
Nikanyanyua sheila na kutokana na kudhohofika kwake kwa mwili haikuwa ngumu kwangu kumbeba hadi tukafika kwenye kwenye moja ya ofifisi na kuwakuta vichaa wakiwashambulia manesi waliomo ndani ya ofisi.Hali ya hospitali imechafuka kupita maelezo madaktari wanashambuliwa na vichaa ambao wamepandwa na hasira.Kwa bahati nzuri nikaona gari moja ya waogonjwa amayo imesimama nje kwenye maegesho huku dereva wake akichomolewa kwenye gari na kuanza kupewa kipigo kama ilivyo kwa wahudumu wengine wa hospitali ikiwemo walinzi.
 
Hapa ndipo nikagundua kuwa vichaa tunafahamiana kwa maana kwa kila nilipo pita huku nikiwa nimembeba sheila hapakuwa na anaye nigusa tofauti na wanapo muona muudumu wa hospitali hii.Nikafanikiwa kufika kwenye gari la wagonjwa nakumuingiza ndani ya gari sheila na kwenda upande wa dereva na kuanza kutafuta fungua na sikuweza kuiona ikanibidi nishuke na kuunza kuupapasa mwili wa dereva ulio lala pembezoni mwa gari na kwabahati nzuri nikaiona funguo kwenye mfuko wake wa suruali.
Nikawasha gari na kuondoka hukiwasaidia vichaa kutoka ndani ya hospitali hii baada ya kuligonga geti lililokuwa kimefungwa.Kutokana sikuwa ni mwenyeji sikujua ni wapi nielekee ili kumuwahisha sheila hospitali.Nikasimamisha gari pembezoni mwa arabara huku likiwa linawaka ving’ora na kuichukua simu iliyopo ndani ya hospitali na kuanza kubuni namba ya baba
 
Kwa mara ya kwanza ikapokelewa na mwanamke ambaye hata lugha hatulewaa na nikajua nitakuwa nimekosea,nikajaribu kufikiria namba nyingi ambazo zinaweza kufanana na namba ya baba na pia namba niliyo ipiga ikapokelewa na kijana na akaanza kumwaga matusi alipoona sizungumzi kitu chochote baada ya kusema haloo.Nikajaribu zaidi ya mara saba nipo kumbukumbu ya namba za baba ziliponijia vizuri kichwani na nikaipiga ikaita kwa muda kisha ikapokelewa
“nani mwenzangu?”
Ilikuwa ni sauti ya baba na kidogo tabasamu likanijia usoni
“mimi eddy”
“eddy……!!”
 
“ndio ni mimi baba ninaomba msaada wako”
Upo wapi mbona makelele ya king’ora?”
“nipo kwenye gari ya wagonjwa nimetoroka hospitalini ila mimi sio kichaa kama ulivyo dhania”
“ngoja kwanza umesema upo wapi?”
“mimi hapa wala sipajui ila kuna magorofa mafupi mafupi hii na kuna magari mengi yamesimama pembeni”
“umesema upo kwenye gari ya wagonjwa?”
 
“ndio”
“wewe ndio dereva ua kuna dereva?”
“mimi ndio dereva”
“sasa angalia kwenye upande wa kusoto kuna kijitivii kidogo….”
“ndio nimekiona”
“kiwashe kama hakija washwa na kwenye sehemu ya chini yake kuna batani nane umeziona”
“ndio” 
 
“minya batani iliyo andikwa map”
Nikaiiminya batani ambayo baba aliniambia na ndani ya sekunde kadhaa kukatokea ramani yenye mistari mingi mingi huku kukiwa na kialama chekundu kikiwa kina waka waka
“inakisoma vipi hiyo ramani?”
“inasoema cape town, western cape city”
“subiri tunakuja sasa hivi”
 
Nikakata simu na kuzima gari na kufungua kijidirisha kilichopo nyuma ya siti yanga na kumuona sheila akiwa amejilaza huku akipumua kwa shida kidogo nikapata matumaini.Ndani ya nusu saa gari mbili zikasimama mbele ya gari nililipo na mtu wa kwanza kushuka ni baba na moja kwa moja akafika kwenye gani na akaonekana kunishangaa jinsi damu zinavyo nivuja.Watu wake wakanitoa ndani ya gari
“baba kuna mtu mwengine huku nyuma”
“ni nani?”
“rafiki yangu”
 
Nikahakikisha wamemshusha sheila na kumuingiza ndani ya gari ndio na mimi nikaingia.Ndani ya gari nikajikausha kimya hadi tukafika kwenye moja ya hospitali.Madaktari wakanichukua na kuniingiza kwenye chumba kingine na sheila akaingizwa kwenye chumba kingine kwa ajili ya matibabu.Matibabu yangu hayakuchukua muda sana japo nimeumia ila kidogo ninaafadhali ni tofauti na sheila.
“eddy ni kitu gani kilikupata?”
“wapi?”
 
“hadi ukawa kama umechanganyikiwa?”
“baba kusema ukweli sijachanganyikiwa ila kuna kitu nilikuwa ninakiitaji kukifanya ili niweze kumpata mtu ambaye anaweza kumjua mama ni wapi alipo?”
“una taka kuniambia kipindi chote hicho ulikuwa ukiigiza?”
“ndio ila lengo langu limefanikiwa?”
“kwanza mama anaendeleaje?”
“mama yako hadi sasa hivi bado hajapatikana japo wale watu ambao niliwapa hiyo kazi wanasema kazi yao inaendelea vizuri”
 
“sasa baba hivyo wanavyo sema kuwa inaendelea vizuri si uongo huo,mimi ninavyo jua kuwa kazi ikiendelea vizuri ni kwamba kuna majibu ya uhakika na wanacho kifanya…….Baba ninatambua fika kuwa wewe unamchukia sana mama kwa sababu ya aliyo kufanyia..Ila kwangu mimi ni tofauti kabisa na wewe ninampenda mama yangu na yeye ndio kila kitu kwangu”
 
Nilizungumza kwa sauti ya ukali kidogo iliyo jaa uchungu kiasi kwamba baba akabaki akitazama chini pasipo kunijibu
“baba….Lengo langu kubwa ni wewe na mama mupatane,musameheane muwe kitu kimoja kumbuka kuwa mimi ndio mtoto wenu wa pekee.Mama hana mtoto mwengine…..Wewe huna mtoto mwengine au unafurahia maisha ya manyanyaso na  yule mwanake mwengine……baba simama kama baba uiokoe familia yako achana na nini kilitokea kati yako wewe na mama.Mimi peke yangu baba nitashindwa bado mimi ni mdogo nahitaji maelekezo kutoka kwenu kwanini baba inakuwa hivyo”
Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakinimwagika baba akainyanyua sura yake na nikashuhudia kwa mbali machozi yakimlenga lenga.
 
“eddy samahani mwanangu sikuweza kulifwatilia hilo swala la mama yako bado ninamchukia sana kupita kitu kingine chochote dunia…niangalie mimi leo hii nimekuwa ni kilema wa kila kitu maishani mwangu.Na kama sio pesa mimi leo hii nisinge weza kutembea…..”
“baba baba kumbuka mama alikubebea damu yako miezi tisa…..”
 
“alinitenga mbali na damu yangu.Alinifanya nisiione damu yangu na aliniulia damu yangu ni nini ambacho eddy mwangu utaniambia nikakuelewa juu ya mama yako”
“haya kama baba au wewe unafurahia kuishi maisha ya kuonewa yule mwanamke asiye na heshima anakazi ya kutembea na waanya kazi wako….?”
“mama yako ndio chanzo wa hayo yote mwangu………mimi sina nguvu za kumfurahisha mwanamke na sindano niliyo chomwa ndio imenipelekea kuwa hivi”
 
Nikabaki mdomo wazi huku nikimuangalia baba kwa macho ya mshangao hulu machozi yakinitiririka.
“eddy anacho kifanya yule mwanamke ni haki yake…..Tangu mimi nimchukue sijawahi kufanya naye chochote….Ndio maana mara ya kwanza nikakuambia kuwa mama yako ni katili sana na mimi ninajua kila kitua anacho kifanya mke wangu”
 
“oohh baba kwanini eeehee umemchukua wa nini sasa yule mwanamke?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa unyonge wa hali ya juu
“eddy nilihitaji kuficha aibu yangu kama mtu mwenye pesa zake”
Nikajukuta ninakosa la kuzungumza na kumfanya kunyanyuka kwenye kiti alicho kaa kilichopo pembezoni mwa kitanda changu cha hospitali kisha akanifwata kwenye kitanda nilicho kaa kisha na yeye akakaa
 
“eddy nakuomba unitunzie siri hii ambayo sipendi mtu yoyote aijue zaidi ya yako wewe na yule mwanamke”
“nitakutunzia baba yangu lakini nakuomba yule mwanamke aondoke pale nyumbani”
“eddy siwezi kuondoka kwa maana atanichafua sana kwani siri yangu sio hiyo niliyo kuambia”
“kwani kuna siri nyingine zaidi ya hiyo?”
“ndio”
 
Ikanibidi nikae vizuri kitandani nimtazame baba huku nikiwa na hamu ya kusikiliza ni nini anaco taka kuniambia
“kipindi ambacho nilichomwa sindano ya sumu madaktari wakanitoa sehemu zangu za siri ili kuepuka kupatwa na ugonjwa wa kansa…..Ila wakanishauri kitu ambacho sikuweza kubisha kwani ningekataa nisinge weza kuwa hai hadi leo”
“kitu gani hicho?”
 “wakalinipandikiza sehemu za siri za jinsia ya kike kwahiyo nipo sawa na mwanamke……”
 
Moyo wangu ukapiga pwaaaaa huku macho yangu nikihisi yakitaka kunichomoka usoni kwani katika maisha yangu sikuwahi kusikia kitu kama hichi ambacho baba yangu mzazi ndio ananiambia.Kulia ninatamani kuzungumza ninashindwa nikawa kama nimegandishwa kwenye tv.Mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa nguvu kiasi kwamba moyo ukaanza kuniuma
 
“eddy…..Eddy”
Baba aliniiita kumsikia ninamsikia ila kuitikia nikajikuta nikishindwa kwani kuna kitu kimenikaba koo kiasi kwamba hata kufumbua mdomo ni shuhuli pevu kwangu.Akaingia nesi akiwa ameshika kisahani cha bati huku kikiwa na vichupa pamoja na bomba la sindano hadi anaviweka juu ya meza ndio kidogo nikaanza kurudi kwenye hali yangu ya kawaida.Baba akanyanyuka na kutoka nje ya chumba na ni nikabaki na nesi na akaniomba nilale kifudi fudi na akanichoma sindano ya kutuliza maumivu kabla hajatoka nikamzuia.
 
“ehee”
“kuna dada mmoja nilikuja naye anaendeleaje?”
“yupo vipi vipi?”
“amekondeana kidogo na mwili wake kidogo umejaa makwaruzo”
“ahaa…yule anaendelea vizuri tuu japo kidogo madaktari wanadai kuwa amepoteza kumbukumbu zake”
“eheee haya asante”
 
Nesi akatoka na kujikuta akili yangu ikikosa hata cha kufikiria na ndani dakika kumi nzima sikuweza kuwaza kitu chochute.Nikajinyanyua kitandani na kuufungua mlango wa chumba na kuchungulia nje na sikumuona baba wala walinzi wake ambao aliwaacha nje.Nikatafuta sehemu yanye viti vya watu kupumzika nikapumzika huku mara kwa mara macho yangu yakielekea mlangoni mwa chumba changu,nikamumba jamaa mmoja gazeti lake baadaya kuona taarifa ya michezo iliyo nivutia juu ya timu ya brazili kupigwa goli saba kwa moja na wajerumani.Kidogo akili yangu ikaanza kuchangamka kila nilipo yatazama makatuni yanayo fanana na wachezaji wa kibrazili yaliyo chorwa kwa utaalamu mkubwa ambao mtu ukiyatazama lazima ucheke
“ndugu mbona unacheka?”
“ahaa ni hawa makatuni walio chorwa humu kwenye hiili gazeti ndio wananifurahisha”
“ahaa”
 
Nikiwa nineandelea kusoma gazeti nikamuana jamaa aliye valia nguo za udaktari akiingia kwenye chumba changu na kwa haraka kumbukumbu ya wale watu walio mteka mama ikanijia kwani kichwa chake amanyoa upara na nimweusi sana.Akakaa ndani kwenye chumba kama dakika mbili kisha akatoka huku macho yake yakitazama huku na huku na ikanibidi kwa haraka nipandishe gazeti juu na kuiziba sura yangu.Nikajikaza nisitetemeke kwa woga ili jamaa mwenye gazeti lake asigundue kitu chochote kinacho endelea.
 
“hembu ninaomba gazeti hilo”
“ehee”
“naliomba mara moja kuna namba ya simu nimeiandika kwenye moja ya kurasa hapo sasa sijajua ni kurasa ipi niliiandika”
 
Jamaa akazidi kunichanganya kiasi kwamba nikajikuta nikiling’ang’ania kwama langu hadi jamaa akaanza kunishangaa.Nikachungulia na kumuona jamaa akizungumza na mmoja wa manesi nahisi anamuuliza ni wapi nilipo na kwa ishara nikagundua nesi alimjibu kuwa hajui ni wapi nilipo kwenda kisha jamaa akaondoka kidogo nikashusha pumzi na kumpa mwenyewe gazeti lake huku nikinyanyuka nikilichungulia jijamaa na nikamshuhudia akijichanganya kwenye watu wanao toka nje.Nikaanza kupiga hatua za kwenda kumtazama ni wapi alipo elekena nakumkuta akizungumza na mwanamke mmoja ambaye nikamtambua kuwa ni emmy.
 
Wasiwasi ukaanza kunijaa kiasi kwamba amani ikatoweka moyoni mwangu kwani sikujua wamejuaje kuwa mimi nipo hapa kwenye hii hospitali.Wakaendelea kuzungumza kisha wakaanza kupiga hatua za haraka kurudi ndani.Nikajificha kwenye ya ukata na wakapitiliza na wote wakaingia kwenye chumba changu na baada ya muda wakatoka na kila mmoja akaenda upade wangu huku emmy akija upande wangu na macho yake yakawa na kazi ya kuwachunguza watu waliomo kwenye sehemu za kupumzikia.Nikaanza kupanda ngazi za kwenda gorofani na kwabahati mbaya emmy akaniona na ikanilazimu niweze kuongeza mwendo wa kupandisha ngazi na yeye akafanya hivyo hivyo.
 
Nianza kukimbia kwenye kordo iliyo ndefu na yenye vyumba vingi na sehemu hii haina watu kabisa na emmya naye akazidi kuongeza mwendo wa kukimbi na kwabahati mbaya mbele yangu ndipo mwisho mwa wa ukuta na hapakuwa na sehemu yoyote ya kukunja zaidi ya vyumba vilivyopo pembezoni.Nikashika kitasa cha chumba kimoja na kukuta kikiwa kimefungwa na ikanilazimu kukimbilia kwenye chumba cha mbeleni ambacho ni cha mwisho kwenye hii kordo na kwa bahati nzuri nikakuta kipo wazi na kitu cha kwanza kukiona ni bomba la chuma linalo tumika kuning’inizia dripu lililo anguka chini huku pembeni kukiwa na mgonjwa akiwa amemelala sakafuni huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na shuka.Nikaliokota bomba na kuchomo kipande kimoja na nikajianza kwenye mlango.
 
Taratibu mlango ukaanza kufunguliwa huku mdomo wa bastola ukiwa umetangulia mbele.Kwa haraka nikaipiga mikono ya emmy kwa kutumia bomba na bastola yake ikaanguka pembeni,nikarusha bomba ili limpiga usoni ila akaikwepa na sikujua amelichukuaje chukuaje mikononi mwangu na nilicho kistukia mimi ni mikono yangu ikiwa haina chochote.Ikawa ni kazi ya mimi kuanza kuyakwepa mabomba anayo nirushia japo kuna baadhi yalinipata vizuri ila nikajikaza na nikabahatika kumpiga ngumi ya pua na kumfanya ajishike pua na ikawa nafasi yangu kumshambulia kwa ngumi za fujo amabozo mara nyingi tunaziita ni ngumi za mtaani kwa maana hazina mfumo maakumu.
 
Emmy akashindwa kuhimili mashambulizi yangu kiasi kwamba akaanguka chini na nikaendelea kumshindilia magumi mfululizo yalio changanyikana na uchungu kwa uzalilishaji walio ufanya juu ya mama yangu.
 
“yupo wapi mama yangu?”
“yupoo yuupo?”
Nikaishusha ngumi kwa kasi kabla haijafika usoni mwake akaniomba huku machozi yakimwagika na damu zikimtoka kwenye maeneo ya kwenye jicho.
“usinipige usinipige eddy,mama yako yupo hapa hapa afrika kusini?”
“eneo gani?”
“kwenye hii hii hopitali ika kwa chini ndipo kuna handaki…”
 
Nikashtukua kitu kizito kikitua kichwani kwa nyuma yangu na nikaanguka pembeni na macho yangu yakaanza kuingia ukungu na kwa mbali nikaliona jinamaa lenye upara likiwa limesika bomba nililokuwa nimelitumia kupambana na emmy na nikashuhudia akitoa bastola yake na kuikoki na macho yangu yakafumba na sikujua ni nini kilicho endelea....


                             ******sory madam******(36)
   
......Nikaanza kusikia kwa mbali sauti ya vyuma vikigogwa kila nilipo jaribu kufumbua macho kutokana na ukungu ulio tawala kwenye macho yangu,nikatingisha kichwa ili kuyaweka macho yangu sawa ili kuweza kuona kitu kilichopo mbele yangu,nikashuhudia watu wengi wakiwa wanaendelea na shuhili za utengenezaji wa magari yaliyo aribika.
Nikasimama na kuhisi maumivu kwenye kichwa changu na nikajaribu kupiga hatua mbili mbele na nikastukia kitu kikinizuia kwenye mguu na nilipo chunguza vizuri nikagundua ni mnyororo ndio unao nizuia na umefungwa kwenye mguu wangu wa kuliaa.Hakuna aliye shuhulika na mimi na kila mmoja akawa anaendelea na shughuli yake na kila nilipo jaribu kumuongelesha aliye pita karibu yangu hakunisemesha kitu cha aina yoyote
 
Nikaaendelea kulichunguza eneo hili na kugundua ni gereji kubwa kwa maana kila eneo limejaa magari yanayo tengenezwa na yaliyo na tayari kwa matumiazia.Baada ya muda watu wawili wanye vifua vikubwa wakanifwata sehemu nilopo na kunifungua myororo  na tukaingia kwenye kitorori kinacho pita kwenye reli na tukaondoka na kuondoa kwenye eneo tulilopo huku tukupita kweye miaamba iliyo pasuliwa na sikujua ni wapi wanapo tupeleka na kila nilipo waomba wanieleze ni wapi tunapo elekea wakabaki wakinitazama huku kitoroli tulicho panda kikizidi kuongeza kasi.
Ndani ya muda mchache tukafika sehemua ambayo nikakuta watu wengi wakiwa matumbo wazi,huku miili yao ikiwa imedhohofika kiasi kwamba wanatia huruma na wengi wao wanafanya kazi ngumu za kupasu miamba na wamechanganyikana wanaume na wanawake.Miili ya watu hawa imechanika chanika kama ilivyo kwa sheila.
 
Wakanishusha kwenye kitorori na tukaanza kupandisha kwenye mawe yaliyo tengenezwa kama ngazi na kila nilipo pita watu nilio wakuta ndani ya hili pango kubwa wakawa na kazi ya kunisikitikia kiasi kwamba nikaanza kupata wasiwasi na walinzi waliomo kwenye hili pango wakawa na kazi ya kuwachapa kwa kutumia mkia wa taa kila mtu aliye jaribu kuniangalia.Tukaingia kweny moja ya kibanda kilicho jengwa na mawe na kukutana na jitu lililo jazia mwili na akawaamrisha wanikalishe kwenye kiti na kuwaomba jamaa walio nileta kunitoa nje.
 
“eddy” aliniita na sikujua jina langu amelijuaje
“umelijuaje jina langu?”
“hahaaaa ni kitu rahisi sana kulijua jina lako kwa maana wewe tumekutafuta kwa muda mwingi sana hadi leo tumekupata kwangu ni furaha kubwa sana”
“wewe nani na unampango gani na mimi?”
“mpango wangu kwako ni ule”
 
Jamaa akanyoosha kidole kwenye kiio na kunionyesha watu wanaoendelea na kazi ngumu ya kupasua miamba kwa kutumia yundo huku wakiwa wamejaa vumbi jingi hata sura zao zikiwa hazionekanani vizuri.
“kuanzia sasa wewe utakuwa ni mtumishi wa humu ndani”
“wewe unaumwa nini hembu nirudisheni sehemu muliyo nitoa”
 
Jamaa akagonga meza yake na wakaingia majamaa nilio kuja nao kisha wakaninyanyua kinguvu na kunivua shati langu na kubakiwana suruali yangu kisha wakanitoa ndani ya ofisi huku wakiwa wemeibeba juu juu.Wakanikabidhi kwa askari mmoja ambaye anaonekana ndio mkubwa wa humu ndani na moja kwa moja askari niliyo kabidhiwa kwake akanipeleka kwenye mango jengine huku akiwa amenibebe begani,nikakuta msari mrefu wa watu wakiwa wamepanga mstari na jamaa akaniangushia nyuma ya mtu wa mwisho kwenye mstari huu kisha akaondoka.
 
Nikachungulia mbele na kuwaona watu hawa ambao kidogo wanaonekana ni wapya kama mimi.Nikaanza kuona kusikia kelele za watu waliopo mbele wakiaza kupiga kelele wakionekana kupata maumivu makali ikanibidi niweze kuchungulia mbele kuona ni kitu gani kinachoendelea,nikawaona watu wawili wakiwa wanalazimishwa kulishwa vitu vinavyofanana na makaa ya moto huku midomo yao ikiwa imeminywa na mijitu mikubwa myeusi ambayo kusema kweli yanatisha kupita maelezo.
Mapigo ya moyo yakazidi kwenda mbio na kila muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mstari ulivyo zidi kusogea mbele na kusema kweli sikuweza kuona sehemu yoyote ya kutoreka kwa maana katika kuta zote za pango kuna vibanda vya askari wakiwa na bunduki mikononi mwao na kila aliye jaribu kukimbia alizawadiwa zawadi ya risasi na huo ndio unakuwa mwisho wa masha yake.Wakasalia watu watano kutoka mimi nilipo na wengine wote walio pita wakawa tayari wamelishwa makaa ya mawe na wamepelekwa kwenye moja ya chumba ambacho sikujua  ni nini kinacho endelea.
 
  Tukabaki watu wawili kwenye mstari nakamshuhudia mtu aliyopo mbele yetu akachiruzikwa na na mikojo kiasi kwamba mwili wake mzima ukawa unatetemeka kiasi kwamba hali ya kutokwa na haja ndogo ikaamia na kwangu na bila ubishi nikashindwa kujizuia na mimi nikajikuta nikilowanisha suruali yangu.Gafla tukasikia filimbi zikipigwa kwa nguvu kutoka sehemu ambayo tuliwaacha watu wanao fanyishwa kazi,ikawalazimu mijamaa wanao walisha watu makaa ya mawe kutuacha na kukimbilia sehemu zinapotoka kelele za filimbi.
Kwa haraka na nikachunguza sehemu zenye vibanda vyenye askari nikagundua wapo bize katika kwenda sehemu zinapo tokea kelele.Nikakimbia kuelekea sehemu zenye kelele na kwabahati nzuri sikuweza kukutana na askari yoyote.Nikakuta hali ya mvurugano kati ya askari na watu wanao tumikishwa humu ndani ya pango,miili mingi ya watumwa ikawa imelala chini ikiwa inavuja damu kutokana na kupigwa risasi na askari waliopo ndani ya pango hili.
 
Watumwa wengine waoga wakaanza kulala chini huku mikono yao wakiwa wameiweka kichwani,nikashuhudia mwanamke mmoja akiwa amelazwa chini akipigwa kipigo kikali na askari walili wanao onekana kuwa na hasira kali sana.Roho ya huruma ikaniingia na kujikuta nikianza kukimbia na kuwakumba watu waliopo mbele yangu na kujikuta nikisimama gafla huku macho ni kiwa nimeyatoa kiasi kwamba hasira ikazi kunipanda hii ni baada ya kumkuta ni mama yangu ndio anaye pigwa na askari hawa wanao onekana hawana huruma kabiasa wa watumwa walipo ndani ya hili pango....
 
 Itaendelea....
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 35 & 36 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 35 & 36 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 21:28:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.