RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 31 & 32 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia...
Emmy akanikaribisha kwenye sehemu anayo ishi ambayo yenye vitu vingi vya dhamani ya hali ya juu.Taratibu emmy akaanza kuvua nguo zake moja baada ya nyingine na kunifanya nibaki nikiwa nimemshangaa kwani sikujua ana maana gani na imekuwaje amevua nguo mbele yangu na kubakiwa na chupi wakati mimi na yeye hatuna mahusiano ya namna yoyote

Endelea...
Emmy akachukua taulo na kujifunga kisha akaingia bafuni na kuniacha mimi nikiwa nimekaa kwenye sofa nikiyatadhimini mazingira ya ndani kwake.Baada ya muda kidogo emmy akatoka bafuni.

“umeshindwa hata kuwasha tv?”
“ahaa hakuna tatizo sana”
“ok ngoja nivae nguo tuelekee hospitalini ukamuone mama”
“sawa”
“ila unajua wodi aliyo lazwa?”
“hapana siijui”
“ok basi tutajua huko huko”

Emmy akaingia ndani kwake na akatoka akiwa amevalia mavazi mazuri kiasi kwamba tamaa za mapenzi zikaanza kunitawala na kujikuta nikimtazama emmy kwa macho ya matamanio
“eddy twende zetu”
“mmmmm”
“twende zetu mbon unanishangaa?”
“ahaa hakuna kitu”

Nikanyanyuka na nikatangulia kutoka nje ila kutokana na baridi kali ikanilazimu kumuomba emmy koti na akarudi ndani na kunichukulia koti lake kubwa na sote tukaingia kwenye lifti na kushuka chini gorofani.
“twende huku kwenye maegesho ya magari”
Tukafika sehemu yenye maegesho ya magari mengi na emmy akafungua gari moja na kuniomba niingie.Safari ikaanza huku kila mmoja akiwa kimya ndani ya gari ila emmy akaamua kuvunja ukimya.

“hivi tanzania wewe unafanya kazi?”
“mimi ni mwanafunzi wa a leve bado”
“ohh kumbe unasoma?”
“ndio”
“kombi gani?”
“pcb”
“mungu wangu pcb wewe....Mbona unaonekana kama hkl?”
“hahaa pcb  halisi...Aafu mbona ndege leo imetua kwenye uwanja wa maputo international airport imekuwaje kutokana tumetua mozambique?”

“ndege ilipata itilafu kwa watu kama sisi tunao jua ndio tumegundua hilo ila ukiwa ni mgeni huwezi kujua kama ndege imeshindwa kuendelea na safari”
“sasa si wangetulipa fidia kwa kwa abiria inakuwaje ndege inakuwa haina uwezo wa kumaliza msafara wake?”
“mimi niliamua tuondoke kutokana wewe umeseme unahitaji kumuona mama yako ila kwa walio baki wakisubiria ndege kutengenezwa watakuwa wamelipwa fidia na kama siku ukiondoka utakwenda kupanda ndege uwanja wa kimataifa wa cape town”
“sawa”

Safari ya kwenda hospitalini haikuchukua muda sana hii nikutokana na wingi wa barabara nyingi zinazo punguza msongamano wa magari.Tukafia hospitalini na moja kwa maja emmy akaenda kwenye katabu kinacho onyesha orodha ya wagonjwa waliopo hapa hospitalini na nikamtajia jina la mama kishha akatumi kama dakika tano kulitafuta na akalipata.

“kumbe mama yako ni waziri?”
“ndio”
“twende ukamuone”
“moja kwa moja tukealekea kwenye chumba alicho lazwa mama na kabla hatujaingia nikamkuta askari mmoja akiwa amesimama nje ya chumba alicho lazwa mama

“hamuruhusiwi kuingia humu ndani nyinyi ni kina nani na munahitaji nini?”
“mimi naitwa dokta emmy samson na mfanyakazi wa hii hospitali”
“naomba kitambulisho chako”
Emmy akatoa kitambulisho chake na kumpa askari aliye simama mlangoni na akakisoma kwa muda kisha akamrushu emmy kuingia ndani na mimi nikataka kuingia ndani ila akanizuia kuingia
“na wewe ni nani?”
“mimi ni mtoto wa huyo mama huko ndani?”
“mbona hatuna maelezo ya aina yoyote kuhusiana kama mgonjwa ana mtoto?”

“mimi ni mwanaye unadhani nitafunga safari kutoka tanzania hadi hapa nije kujipendekeza kwa mama yangu?”
Nilizungumza kwa hasira kiasi kwamba watu walipo karibu na eneo la mlango wa kuingia kwenye chumba alicho lazwa wakaanza kunishangaa
“eddy kuwa mpole ngoja nikamuone mama”
“kijana ninakuoma usimame mbali na hili enoa la sivyo nitakuitia walinzi waje wakutoe”
“eddy tafadhali nakuomba uwe mpole nitazungumza na mama na utamuona tu”

Nijaitahidi kutulia hasira zangu na kusimama pembeni kidogo na chumba alicho lazwa mama huku sura yangu ni kiwa nimeikunja.Emmy akaingia ndani ya chumba na baada ya muda akatoka na kumnong’oneza askari kisha kwa ishara emmy akaniita na nikanyanyuka kwa haraka hadi sehemu waliyo simama kisha askari akaniruhusu kuingia ndani.Macho yangu yakatizamana na mama ambaye kwa muonekana hali yake sio nzuri sana japo nimemkuta amaekaa kitako kwa mwendo wa haraka nikamfwata mama na kumkumbatia huku machozi yakinimwagika.

Tukabaki tumekumbatiana na mama ndani ya dakika kadhaa kisha nikamuachia na kuiona sura yake ikiwa imelowana kwa machozi mengi,mama akanishika mashavuni na kunibusu kwenye paji la uso huku akinichunguza sehemu mbali mbali za mwili mwangu na kunifanya nizidi kububujikwa na machozi
“eddy ni nini kilicho kupata mwanagu?”

Mama aliniuliza huku akiwa anabubujikwa na machozi kiasi kwamba nikashindwa kulijibu swali lake hadi ndani ya dakika tano ndipo nikaanza kumuadisia kila kitu kilicho tokea na jinsi baba alivyo nifanyia kiasi kwamb hadi ninamalizia nikamshuhudia emmy akiinama chini huku akitokwa na machozi.
“eddy mwanagu nakuomba unisamehe”
“nikusamehena nini mama?”
“eddy najua siku zote ulikuwa unahitaji kujua ukweli juu ya baba yako na mimi nikawa nimekuficha ila....”
“mama nimesha lijua hilo kuwa pacha wa baba ndio baba yangu”

“nani amekuambia hivyo?”
“mama dunia haina siri tena hili swala nimeambia na mtu baki kabisa tena ni muandishi wa habari”
“basi eddy tuliache hilo mwanagu kwa maana unazidi kunipa uchungua katika hilo”
Ikanibidi nibadilishe mada ya kuzungu na kuzungumza na kuanza kupiga story za kupoteza mawazo hadi mama na emmy wakaanza kucheka ila sikumuambia mama kuhusiana na swala la shule yetu kuingia kwenye matatizo.

“emmy hapa ni wapi kwenye choo?”
“ukitoka hapo nje mkono wako wa kushoto utaona milango miwili imeandikwa toilet”
“ahaa powa”
Nikatoka nje na kumkuta askari akiwa amesimama mbali kidogo na chumba akizungumza na simu akionekana akiwa na mazungumzo ya siri ikanibidi kulitega sikio langu kwa umakini kusikiliza ni kitu gani anacho kizungumza.

“ndii si nimrefu kiasi na mwili wake umejazia kidogo?”
“basi amefika hapa kama lisaa lililo pita”
“amekuja na mwanamke fulani ambaye hapa ni ndakatari”
“basi panda ndege uje kwa maana inavyo onekana mipango yote itakwenda kuharibika”
“sawa mr godwin”
Nikajikuta hata hamu ya kwenda kujisaidi haja ndogo ikakata na kabla hajaguka nikaingia ndani huku nikiwa ninawasiwasi hadi mama akanigundua kwa haraka.

“una tatizo gani mwanangu?”
“mama hivi huju mlinzi mumemtoa wapi?”
“kwa nini?”
“wewe nijibu?”
“huyo amekwa na ubalozi wa tanzania uliopo hapa nchini”
“unauhakika kweli ni mwema?”
“ni mwema kivipi?”
“au kuna siku ambayo baba alisha wahi kuja hapa”
“hajawahi kuja hapa na wala hatambui kama nipo hapa”
“sawa”

Nikatoka nje na kumkuta mlinzi akiwa amesimama kwenye sehemu ambayo tulimkuta kwa mara ya kwanza na akaniangalia kwa jicho la kuiba na mimi moja kwa moja nikaelekea chooni na kumaliza haja yangu kisha nikarudi huku moyoni mwangu nikiwa na wasiwasi kiasi kwamba nikakosa amani kabisa ya kukaa ndani ya chumba alichopo mama na emmy.
“emmy nakuomba mara moja nje?”
“kwema?”
“kwema tuu wewe ninakuomba”

Emmy akatoka na nikamshika mkono hadi sehemu iliyo tulia ambayo si rahisi kwa askari kuniona
“hivi tunaweza kumuhamisha mama hospitali?”
“kwanini?”
“nijibu kama kuna uwezekano wa mama kuhamishwa hospitali ua hakuna?”
“uwezekano upo ila ni hatua zahadi yeye kuhamishwa kwenda hspitali nyingine ni ndefu kwa maana hapa ameletwa na serikali ya tanzania....Ila ni kwanini unahitaji ahamishe kuna nini?”
“nafsi yangu imekosa amani kabisa juu ya mama kuendelea kuwa katika hospitali hii”

“wasi wasi wa nini wakati hapa maaskari wamejaa wengi na hakuna mtu atakaye weza kumdhuru mama na mimi leo nitakaa naye siku nzima humu ndani”
“emmy ninaamini hujui kwa undani hali ya familia yangu pale umesikiliza mamaneno machache wewe mwenyewe umejikuta ukitokwa na machozi sasa sihitaji uweze kulia zaidi ya pale ulivyo kuwa unalia?”
“kwa nini unakuwa unananificha kwa kitu ambacho wewe unakihisi?”
“kwa sasa huwezi kunielewa ila utanielewa”

Nikaachana na emmy na kwenda chumbani kwa mama na kumkuta akiwa anazungumza na madakatari wawili ambao wamejifunga vitambaa vya kijani usini vinavyo fanana na nguo zao walizo zivaa baada ya kuniona mimi wakaniomba nisubiri nje kwa muda.Kusema ukweli nafsi na moyo wangu vikajikuta vikishindwa kuchukua maamuvu ambayo madakatri wameniomba nitoke.Emmy akaingia na akaonekana kuwashangaa madaktari hawa ambao wamejifunga vitambaa jambo ambalo ni tofauti sana kwa madaktari tunao waona kwenye hii hospitali wakiwa wameziacha sura zao wazi.

“nyinyi ni kina nani?”
Madaktari wakatazamana kisha mmoja akajikoholesha kisha akaanza kuzungumza kwa sauti ya kujiamini
“sisi ni madakatari maalumu tumetumwa na serikali ya tanzania kuja kuzileta dawa ambazo zinamsaidia muheshimiwa waziri katika kupona”

“ngoja mumesema kuwa mumetoka wapi?”
“tanzania?”
“dawa mumetumwa na nani?”
“na wizara ya afya”
“hivi nyinyi kama hizo dawa mungeziona zina faida sana si munge mpa mama yangu tangu siku akiwa yupo tanzania akiwa anaumwa”
“hizi dawa kwa hapa hatuna tumeziacha ofisini”
“basi nendeni mukazilete”

Madakatari wakaanza kubabaika kiasi kwamba sote tukabaki tukiwatazama kwa macho makili na hata walivyo toka hawakuga kiasi kwamba wasiwasi wangu ukaanza kupata jibu kwamba kuna mkono wa baba katika swala hili.
“mama ninahitaji tuhame hospitalini kwa maana baba anatufwatilia na nisipo angalia ninaweza kufa”
“kweli mwanangu?”
“basi ngoja nikaonane na daktari mkuu nitakuja muda sio mrefu”

Emmy akatoka ndani ya chumba na kutucha mimi na mama huku akili yangu ikiwa na kazi ya kupanda nini cha kufanya kuweza kumtorosha mama katika hospitali hii.Baada ya nusu saa emmy akarudi akiwa ameongozana na daktari mmoja wa kuzungu ambaye ni mtu wa makamo.

“mama huyu ndio mkuu wangu wa hapa kazini”
Daktari mkuu akaanza kutupa mipango ya kufwata ili tuweze kumuhamisha mama katika hospitali hii jambo ambalo kwa mtazamo linachuku muda mrefu wa siku kama mbili kwani nilazima kibali kiweze kutoka katika serikali ya tanzania na kipitie katika ubalozi wa tanzania ndipo mama aweze kuhamishwa.

“basi tutabubiria hadi kesho”
“mama hadi kesho una uhakika na kitu unacho kizungumza?”
“eddy kila kitu kinakwenda kwa mpangilio wa kiserikali na ukisema uende wewe kama wewe itakuwa ni shida kumbuka kuwa mimi serikalini nina mamlaka na ninachukuliwa kama kiongozi kwahiyo nakuomba uwe mvumilivu mwanangu”
“mama..”
“eddy nielewe......Sawa daktari nimekuelewa nyinyi fanyeni hizo hatua na mukihitaji msaada wangu tutashirikiana”
“sawa”

Emmy na daktari mkuu wakatoka nje na kutuacha mimi na mama huku nikiwa ninamipnago mingine ya kuto kumshorikisha mama.Emmy akarudi ndani na kukaa pembeni ya kitanda alicho lala mama
“eddy unaoenekana wewe ni mbishi sana”
“huyo mwanangu nimesha mzoa ila ana ugonjwa wa hasira kiasi kwamba akiwa anabishana na mtu huwa hapendi kushindwa”

“mama achilia na ugonjwa wa hasira ila kuna hatari ipo mbele yako sasa nyinyi endeleni kuniona kuwa mimi sifai”
Tukaendelea kukaa hadi mida ya saa moja usiku nikamuomba emmy kunielekeza ni wapi ninaweza kupata sehemu yenye benki ya backryas na akanielekeza na haikuwa mbali sana na sehemu hospitali ilipo.

“niwachukulie chakula gani?”
“mimi nina chakula changu maalumu huwa ninaletewa na madakatari wa hapa?”
“emmy?”
“mimi niletee keki na soda ya kopa ya koka”
Nikatoka na kumkuta askari akiwa anatembea tembea huku  na kule akionekana akisubiria kitu fulani kwa hamu
“hivi zamu yako wewe inabadilika saa ngapi?”
“nani mimi?”
“kwani hapa nina ongea na nani?”
“mimi zamu yangu inabadilika saa nne usiku”
“ahaa powa”

Nikaachana na askari na kwenda sehemu aliyo nielekeza emmy na kukuta atm ya benki ya backrays na kuchukua pesa kiasi zitakazo nisaidia katika matumizi madogo ya hapa africa kusini.Nikaingia kwenye mgahawa uliopo karibu na  hospitali na kuagizia chakula ambacho nitaweza kukila na nikatafuta sehemu ambayo ninaweza kuuona mlango wa kuingilia katika hospitli na kabla sija letewa chakula nikaona taksi ikiwa imesimama kisha nikamshuhudia baba akishuka ndani ya gari akiwa ameongozana na wanaume wawili na katika taksi nikamuona sheila akiwa amekaa siti ya nyuma.Kwa haraka nikanyanyuka na kutoka nje ya mgahawa na kutokana na magari mengi ikanilazimu kuvunja seheria za barabara na kujikuta nikivuka kwa haraka barabara na kabla sijamalizia nikashtukia nikikumbwa na gari lililo nirusha na kuangukia pembeni ilipo simama taksi aliyopo sheila
                        *****sory madam*****(32)

Nikatulia chini kwa muda na kumuona sheila akifungua mlango kwa haraka na kushuka ndani ya gari na akaonekana kunishangaa baada ya kunijua ni mimi,nikajaribu kujinyanyua ila nikajikuta nikishindwa kutokana na mguu wangu mmoja kutawaliwa na maumivu makali.Nikastuka baada ya kugundua mguu wangu wa kushoto umevunjika japo kichwani na mikononi nimepatwa na michubuko iliyosababishwa na kuaanguka na kuserereka kidogo kwenye barabara ya lami.Sheila akaoanekana kupigwa na bumbuazi kwani hakuzungumza kitu cha aina yoyote zaidi ya kubaki akinitazama hadi watu walipo anza kukusanyika na kuwaomba wauguzi wa hospitalini kunisaidia,

Nikawawekwa kwenye machela na kuingizwa ndani pasipo sheila kuzungumza kitu cha aina yoyote kwangu,nikaingizwa kwenye moja ya chumba ambacho ni chaupasuaji na kwa haraka nikachomwa sindano za ganzi kwenye mguu wa kushoto ambao umevunjika na kawanipaka mafuta kisha wakamipitishia kifaa maakumu kinachotoa mwanga mwekundu wenye miyonzi mikali huku dakitazama picha inayopita kwenye tv ndogo iliyopo ndani ya hiki chumba wakaona ni sehemu ya ambayo mguu umevunjika na wakaanza kazi ya kunihudumia

Ndani ya lisaa moja wakamaliza upasuaji wao na kunifunga bandeji kubwa kisha majeraha madogo madogo wakayapaka dawa kisha wakanihamishia kwenye wodi kitu ambacho ninakiona ni chatofauti ni huku kufanyiwa upasuaji pasiopo kuchomwa sindano ya usingizi.Sikuweza kupata rafiki wa kunijulia afya yangu na kitu kinacho niumiza sana akili yangu ni jinsi hali ya mama ilivyo na kingine sikujua kama ameweza kusalimika mikononi mwa baba ambaye ndio amekuwa adui yetu namba moja kwenye familia yetu.Sikua ya kwanza ikakatika huku nikiwa sijui kitu kinacho endelea ila zaidi nikawa ninahudumiwa na kupewa chakula na wauguzi wa hospitalini.

Wiki moja ikakatika na hali yangu ikaendelea kuwa nzuri zaidi na nikaanza kufanyishwa mazoezi ya kutembea na siku hii nikamuomba muuguzi kunipeleka kwenye sehemu kilipo chumba alichomo mama na hakusita na kwa mwendo wa taratibu tukafanikiwa kufika ila sikuweza kumpata mama na ikanibidi kumuuliza muuguzi huyu kwa lugha ya kingereza

“hivi huyu mama humu ndani amekwenda wapi?”
“mama yupi?”
“kuna mama waziri ambaye alilazwa humu chumbani”
“sijajua labda tukaulize sehemu zenye rekodi ya wagonjwa kwa maana mimi sihusiki katika kitngo hichi na kama unavyo iona hospitali yetu ilivyo kubwa siwezi kuwajua wagonjwa wote”
“sawa dada yangu basi nakuomba unifikishe hiyo sehemu wanayo angalizia orodha ya wagonjwa”

Cha kumshukuru mungu huyu nesi hana makuu zaidi ya alicho kifanya ni kunipeleka hadi sehemu wanayo angalizia idadi ya wagonjwa walipo kwenye hospitali hii na kadri tunavyo litafuta jina la mama kwenye kumputer yao hawakuliona na ikanibidi niweze kuuliza jina la daktari emmy na jibu nililo lipata kutoka kwa mfanyakazi wa ofisi hii ya takwimu za hospitali likazidi kunichanganya
“hapa hospitalini kwetu hatuna jina la daktari anaye itwa emmy na dokta anaye anziwa na herufi ya e ni mwanaume na anaitwa emmanuel”

“kweli huyo daktari hayupo....Mbona ana hadi kitambulisho na kitambulisho kinacho muonyesha kuwa yeye ni daktari wa hii hospitali?”
“wewe ulikutana naye wapi?”
“tanzania na nikapanda naye ndege moja hadi hapa”
“mmmm hapa mulikuja lini?”
“kama wiki moja iliyo pita”
“ngoja kwanza”

Msichana anayehusika na maswala ya takwimu akanyanyua mkonga wa simy ya mezani kisha akaminya baadhi ya namba na kuiweka simu yake sikioni
“kiongozi ninashida moja ninakumba unisaidie”
“kuna tatizo limejitokeza la hawa madaktari feki kuendelea kuivamia hospitali yetu na wanaendelea kufanya matukio ya ajabu”
“basi ninakuja sasa hivi”

Akakata simu na kuniomba niogonzane naye huku nesi anaye nifanyisha mazoezi akinishikilia vizuri na tukaingia kwenye lifti na ikatupeleka hadi gorofa ya tatu na tukaingia kwenye chumba ambacho nikakuta tivi nyingi ndogo ndogo ambazo idadi yake kwa haraka haraka zinaweza kufika hamsini na kila tv inaonnyesha sehemu yake na nikagundua zinaonyesha picha za kamera za ulinzi zilizo fungwa ndani ya hii hospitali
“una rekodi za wiki nzima?”
“ndio ninazo”
“ninaomba utuwekee za siku saba za nyuma”

Jamaa anaye onekana ndio muongozaji wa kamera za humu hospitali akaigeukia tv moja kubwa kama nchi 32 kisha akachuku cd ndogo na kuziingiza kwenye deki ndogo na tukaanza kuangalia video zilizo chukuliwa ndani ya wiki moja  na nikajikuta nikinyoosha kidole changu kwenye moja sehemu hii ni baada ya kujiona nikiingia hapa hospitalini siku ya kwanza nikiwa na emmy na kumfanya jamaa kuisimamisha sehemu hii kisha akaisogeza kwa ukubwa kiasi(zoom) na kuiangalia sura ya emmy ambaye alizidi kunichanganya baada ya kumuona dada wa ofisi ya takwimu akitingisha kichwa huku akiibenua midomo yake
“mmmm hatuna daktari kama huyu”
“kaka hembu peleka mbele”

Jamaa akairuhusi cd kutembea na kuanza kuangalia picha za mbele na kujiona nikiingia ndani ya chumba alichokuwa mama kipindi ninatoka kuzungumza na emmy baada ya kuanza kuhisi hali ya ajabu,video ikamuonyesha emmy akizungumza na askari ambaye alikuwepo pale mlangoni kisha yeye akaingia ndani huku akiitazama camera ya ulinzi iliyokuwepo juu.

“hii ni camera namba 38 ngoja niweke video zake kwani huu ni mkanda wa jumla”
“sawa fanya hivyo”
“na huyo askari hapo ni wa hapa?”
“askari huyo aliletwa na ubalozi wa tanzania kumlinda huyo mama.....Kwani wewe huyo mama ni nani yako?”
“mama yangu mzazi”

Jamaa akaito cd aliyokuwa ameiweka kwenye deki kisha akatafuta cd nyingine ndogo na kuuweka kwenye deki yake na tukaendelea kuona matukio yaliyo endelea eneo la nje ya chumba alicho lazwa mama baada ya mimi kuondoka kuelekea banki.
Tukamuona askari  akipewa soada ya kopo na emmy na akaianza kuinywa baada ya emmy kuingia ndani na baada ya muda akaonekana kama anaumwa na tumbo na akandoka katika eneo la nje ya chumba akielekea sehemu vilipo vyoo na baada ya muda kidogo mlango ukafunguliwa na kumshuhudia emmy akiwa amevalia koti la kidaktari akikisukuma kitanda cha mama huku mama akiwa amefumba macho yake na kulala kama mtu aliye poteza fahamu

Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio huku nikiema kwa hasira na kujikutani nikiyang’ata meno yangu kwa hasira kiasi kwamba nikatamani nipone kwa haraka ili niweze kumsaka emmy sehemu yotote akatakayo kuwepo nchini afrika kusini.Nikashusha pumzi huku nikiwa macho yangu yamebadilika na kuwa mekundu na kujikuta nikikitazama kioo kilichopo ndani ya chumba hichi kinacho nionyesha vizuri sura yangu na kila mtu akabaki akinitazama kwa umakini pasipo kuzungumza kitu chochote
“hemu rudisha hiyo cd ya kwanza”

Jamaa akairudisha cd ya kwanza na kipelea mbele kidogo na kumuona emmy akimuingiza mama ndani ya gari la wagonjwa huku akisaidiana na watu wawili ambao niliwaona wakishuku na baba huku nao kwa sasa wakiwa wamevalia makoti meupe wakionekana kama madaktari.
“kaka hembu simamasha kidogo hape na zoom kwenye kioo cha dereva wa hilo gari”

Jamaa akafanya kama nilivyo muagiza na akaikuza picha ya dereva na kugundua ni baba japa amevalia miwani huku akiwa amebandika ndevu za bandia na kumfanya aonekane kama mtu wa makamo
“kwani flora ina maana hawa jamaa sio wafanya kazi wa hii hospitali?”
“ndio”

“mbona wanavitambulisho kwa maana mimi hili tukio linatokea sikustushwa kwa maana ni jambo la kawaida kwa wagonjwa kuhamishwa hapa hospitalini kwetu”
Nikamshuhudia flora ambaye ndio muhusika kwenye ofisi ya takwimu akikuna kichwa pasipo kuzungumza kitu cha aian yoyote.

“je daktari wenu mkuu yopoje?”
“yupoje kivipi?”
“yaani muonekano wake?”
“ni mweusi kiasi kiasi na sasa yupo captown kwenye kikao cha madaktari wakuu hapa nchini”
“mbona alikuja mzee wa kizungu huyo dada akasema ndio daktari mkuu?”
“mmmm atakuwa amekudanganya kwani ni wiki ya pili daktari mkuu yupo kwenye kikao cha madaktari kama nilivyo kuambia hapo awali”

Sikuwa na lakuzungumza zaidi ya kuumiza kichwa ni jinsi gani ninaweza kumpata mama yangu na moja kwa moja nikajua ametekwa na baba na sikujua ni wapi alipo mpeleka.
“tutawasiliana na polisi kuweza kulifwatilia hili tukio”
“naombeni mufanye hivyo kwani mama yangu ndio kila kitu katika maisha yangu kwa maana nimetoka tanzania kwa ajili yake na mwisho wa siku mambo yanakuwa kama hivi”
“usijali wa hilo”

Nikakaa hospitali zaidi ya wiki nne na nikapona kabisa mguu wangu na kufunguliwa bandeji nililo fungwa.Habari za wapi alipo mama kila nilipojaribu kuwaulizia walio sema watalishuhulikia wakadai bado askari wanaendelea na uchunguzi ambao sikujua utaisha lini
“kaka gharama zako za hospitalini zimesha lipiwa”
“zimelipiwa na nani?”
“aliye kulipia ni yule aliye kugonga na gari na yupo nje anakusubiria?”

Nikaanza kujiuliza ni nani huyu aliye ni gonga na kuwa na moyo wa kujitolea kiasi kwamba amenilipia gharama zote za ajali yangu wakati mimi ndio nilikuwa ninamakosa.Nikatoka nje pamoja na daktari aliye niambia habari hii ambayo kwangu ni nzuri kiasi japo bado akilini nimetawaliwa na wazo la wapi alipo mama.

Daktari akanionyesha mzee mmoja aliye valia koti jeusi la suti na alinipa mgongo kwani anazungumza na simu,ikatulazimu kumsubiria amalize ndio daktari amjulishe uwepo wetu.Baada ya muda akakata simu na kugeuka na kujikuta nikihamaki kwa kiasi kikubwa kwani mtu aliyepo mbele yangu anafanana kabisa na baba yangu ambaye kwa sasa ni adui yangu namba moja.
“habari yako kijana”
“sh...Ikamaoo”

Nilipata kigugumizi cha gafla kiasi kwamba mzee naye akaanza kunitazama kwa umakini huku akionekana kunichunguza kuanzi kichwani hadi miguuni.Daktari akatutizama kwa muda na kuzungumza kitu kilicho tufanya sote tumtimame
“huyo ni mwanao?”

Hakuna aliye lijibu swali la daktari zaidi ya kukaa kimya kimya na tukageukiana na kuendekea kutazama na kadri tulivyo zidi kutazamana ndivyo nilivyohisi ukweli wa maisha yangu juu ya baba yangu kwani kuanzia macho pua midomo na sura hakuna kilicho pishana na mwenzake kiasi kwamba machozi yakaanza kunilenga lenga huku moyoni mwangu nikijihisi amani na furaha iliyo kuba tofauti na ninavyo kuwa na baba yangu gaidi.
“jina lako ni nani kijana?”
“eddy”
“eddy nani?”
“godwin”

Nikastukia mzee akinikumbatia kwa furaha huku akicheka kwa kicheko kikubwa cha furaha na akaninnyanyua juu kidogo na kuanza kunizungusha kisha akanisimamisha na kunitazama tena usoni huku machozi ya furaha yakimwagika na mimi nikajikuta nikiachia basabu pana
“dokta nahitaji vipimo vya dna na huyu kijana”
“sawa ila inabidi na yeye aridhie”
“eddy upo tayari kwa hili?”
“ndio mzee”

Sikuweza kumuita baba moja kwa moja japo tunafanana kwa asilimia 99(tisini na tisa) ila nikahofia endapo majibu yatakuwa siyo sijui sura yangu ningeiweka wapi.Tukaingia kwenye maabara nzuri na yakisasa kisha tukachukuliwa damu na kuombwa kusubiri nje.
“eddy mimi ninaitwa godfrey nani mtanzania japo sasa hivi nina uraia wa hapa arfrika kusini hii ni kutokana na kuishi miaka mingi hapa afrika kusini”

“ahaa sasa ni kwanini uliondoka tanzania ilikuwaje?”
“ni historia ndefu sana iliyo nipata hadi kufikia hapa ni vikwazo na mambo mengi nilipitia ila ninamshukuru mungu hadi leo hii nipo salama”
“ni kitu gani kilicho kupata?”
“ni mambo mengi sana yaliyo nipata na hapa sio wakati muafaka wa kulizungumzia hilo”

Kabla sijamuuliza swali jengine mlango wa chumba cha maabara kikafunguliwa na akatoka daktari aliye tuchukua vipimo vya damu na kutuomba twende naye ofisini kwake ambapo akatupa mikono huku usoni mwake akiwa na furaha
“majibu ni asilimia 100 damu zenu zinafana”

Ikawa ni habari mpya yenye furaha maishani mwangu kwani siku zote kilio changu ni kuhusiana na baba yangu.Baba akanyanyuka kwa fauraha na kunikumbatia huku mkono wake mmoja akiupiga piga mgongoni mwangu,machozi ya furaha yakanibubujika na hata wazo la mama kichwani mwangu kwa wakati huu likafutika kidogo.Baba akatoa simu yake na kupiga namba fulani
“andaa tafrija kubwa na waalike watu wangu wa karibu kwani nina kitu cha kuzungumza nao”
“fanya hivyo na ndani ya lisaa nitakuwa hapo nyumbani”
“waambie ni saa mbili usiku”

Sikujua baba anatoa maagizo kwa mtu gani kisha akatoa kitabu kidogo cha kuchukulia pesa na kuandika kiasi anacho kijua yeye kisha akampatia daktari na nikaondoka huku nikiwa nimebeba baasha yenye majibu yetu ya dna.Tukatoka nje na kulekea eneo la maegesho ya magari na dereva aliye valia suti nyeusi akafungua mlango wa gari aina astorn martin na kidogo dereva akawa ananishangaa.Safari ikaanza huku kila nilipo tazamana na baba tukajikuta tukitabasamu ikiashiria ni furaha iliyotawala kati yetu.

Geti kubwa likajifungua na mbele yangu kwa mbali kidogo nikaliona jumba kubwa midhili ya ikulu na kuna eneo kubwa lenye kila aina ya kitu cha kuburudika pamoja na bustani kubwa zenye maua ya kupendeza sana

“karibu nyumbani mwanangu”
Kwa wingi wa walinzi walioo kwenye eneo hili hadi nikaanza kuogopa japo ni baba yangu ila sikujiamini sana juu ya usalama wangu
“karibu sana nyumbani eddy”
“asante baba”

Tukashuka kwenye gari huku macho yangu yakitazama tazama pande zote za sehemu tuliyupo.Mlango wa kuingilia ndani ukafungulia na macho yangu yakakutana na seble inayoendelea kupambwa na wafanyakazi na akashuka mama mmoja wa kizungu kwenye ngazi na kuja kumkumbatia baba kisha akambusu mdomoni na mama huyo akabaki akinishangaa

“huyu ni nani?”
“mwanangu”
Mama wa kizungu akanipa mkono kwa dharau kisha akaondoka huku akionekana kukasirika kwa uwepo wangu katika nyumba hii hadi nikajihisi vibaya
“eddy mwanangu karibu na jisikie upo huru na mwenye amani kwa maana hapa ni kwako”
“asante baba yangu”

Niliitikia kwa sauti ya kinyonge ila moyoni mwangu nikaanza kuhisi kuna mapambano yatakayo endelea kati yangu na huyu mama wa kizungu.Tukaongozana hadi kwenye chumba kikubwa chenye mali nyingi za dhamani na baba akanikaribisha kwenye moja ya kiti kilicho tengenezwa kihalisi na yeye akakaa kwenye sehemu nyingine

“una hitaji kinywaji?”
“hapana”
“sawa eddy kwanza ninakuomba unisamehe kwa kile ulicho kiona pale mlangoni”
“bila samahani kwani yule ni nani?”
“yule ni mke wangu wa ndoa ambaye nimefunga naye ndoa miaka mitano iliyo pita”
“aaaahaa sasa mbona ameonekana kuchukizwa baada ya kuniona?”

“ahaa nahisi hakutegemea kuupata ujio wako leo kwani hata mimi sikuwahi kumuambia kuwa mimi nina mtoto”
“sawa na yeye ume zaa naye?”
“hapana na sina mtoto mwengine zaidi yake japo yeye naye ana mtoto wa kike hayupo hapa yupo johnsburg anasoma chuo”

“mama yako hivi hajambo?”
“siwezi kujiu kama hajambo au anaendeleaje kwa maana alikuwa yupo hospitalini na amatekwa?”
“ametekwa na nani?”
“ametekwa na baba?”
“ina maana kaka godwin anaweza kumteka mke wake?”

“baba hiyo ni historia ndefu sana,na chanzo kikubwa cha mimi kuja huku ni yeye kwa maana alikuwa amelazwa kwenye ile hospitali uliyo nikuta”
“duu kweli malipo ni hapa hapa duniani?”
“kwa nini baba?”
“mama yako ni katili sana tena zaidi ya sana japo usoni mweke ni mwama kupitiliza”
Maneno ya baba yakanicha mdomo wazi huku nikishangaa nisijue ni kwanini amesema mama yangu ni katili sana

 Itaendelea.... 
RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 31 & 32 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 31 & 32 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea ) Reviewed by WANGOFIRA on 21:25:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.