News Alert!! BASI LA NEW FORCE LA DAR - SONGEA LAPATA AJALI NJOMBE,WATU KADHAA WAPOTEZA MAISHA

ajali songea 
Taarifa tulizozipata hivi punde leo Jumatatu,Septemba 19,2016 ni kwamba Basi la New Force kutoka Dar es salaam kwenda Songealimepata ajali kwa kupinduka maeneo ya Kifanya kilomita kadhaa kutoka mkoani Njombe.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja usiku wa Septemba 19,2016 ambapo inaelezwa kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Madaba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe ACP Prudenciana Protas amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,yuko eneo la tukio na ameahidi kutoa taarifa rasmi hapo baadaye.

Tutawaletea taarifa kamili hivi punde
News Alert!! BASI LA NEW FORCE LA DAR - SONGEA LAPATA AJALI NJOMBE,WATU KADHAA WAPOTEZA MAISHA News Alert!! BASI LA NEW FORCE LA DAR - SONGEA LAPATA AJALI NJOMBE,WATU KADHAA WAPOTEZA MAISHA Reviewed by WANGOFIRA on 14:43:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.