MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP), WAANZA MIKAKATI YA KUHAMASISHA ELIMU.

Mratibu wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari Kitongani.


Wazazi na wanafunzi Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamepongeza kwa dhati jitihada zinazofanywa na uongozi wa mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP). Kwa kuamua kupita na kutembelea Shule za sekondari zilizo katika wilaya ya kigoma mjini na kuhamasisha wanafunzi watimize majukumu yao kwa kutambua wana mchango mkubwa kwa taifa.

Akipongeza juhudi hizo Peter Juma ambaye ni mmoja wa wazazi alisema kuwa ni jambo jema kuwaona vijana wakitiana moyo hasa kimasomo. Maana ni mara chache sana kuona vijana kama hawa kujitoa na kukumbuka vijana wenzao hasa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari na kuwatia moyo na ili wasome kwa bidii.

Nae Mratibu wa mtandao huo mkoa wa Kigoma Abdul omary Nondo, alisema kuwa mtandao huo unafahamu umuhimu wa elimu, na katika mtandao wao wana idara ya haki na wajibu wa wanafunzi, ili kutetea haki za wanafunzi.

Pia ameongeza kuwa  "lazima tuangalie kama wanafunzi wanatekeleza wajibu wao ipasavyo maana walimu kila siku wanatekeleza wajibu wao wawapo shuleni hivyo ni wajibu na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu ili waweze kujifunza mambo mengi ambayo yataleta mapinduzi kwenye elimu hususani kidato cha nne ambao muda si mrefu watahitimu masomo yao.

Aliongeza kwa kuwasihi wanafunzi hao kuwa na Nidhamu ambayo itafanya waweze kusoma pasipo kuwa na usufumbufu wowote ule kutoka kwa walimu, wazazi na jamii kwa ujumla. na pia waepuke makundi mabaya ambayo hayana msingi wa kuwajenga kitaaluma.

 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Kitongani Moshi Juma alitoa pongezi za dhati kwa mtandao huo kwa kuwapa elimu ya utambuzi ambayo imewajengea ujasiri na kuwasisitiza umuhimu wa kusoma kwa ratiba ili aweze kuongeza ufaulu wake.

Mtandao huu kwa sasa umeenea karibu mikoa yote ya Tanzania bara, ambapo viongozi wake mbalimbali wanafanya ziara mashuleni wakilenga kuwapa elimu ya kujitambua wanafunzi ili waweze kubadili fikra na kujenga mtazamo chanya katika maisha yao ya shule.

 Pamoja na jitihada hizo bado mtandao huu unakabiriwa na changamoto ya Fedha ambapo wajumbe wa mtandao huu ujitolea fedha zao mfukoni ili kutekeleza shughuli za mtandao na kuhamasisha wanafunzi mashuleni.  Na kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuwaunga mkono ili waweze kujenga Tanzania Mpya na yenye vijana wasomi wenye tija kubwa kwa taifa hili.

kwa sasa wanapatikana SINZA  at GROUP ZINZA DAR,
P. O.BOX 110024,
Phone number :0765443728/0652068952/0764254650.
Email :tsnp.student@yahoo. com
Facebook :sauti ya wanafunzi Tanzania.
MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP), WAANZA MIKAKATI YA KUHAMASISHA ELIMU. MTANDAO WA WANAFUNZI TANZANIA (TSNP), WAANZA MIKAKATI YA KUHAMASISHA ELIMU. Reviewed by WANGOFIRA on 11:52:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.