Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam


Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.

Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari   ya Noah.

Taarifa  kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.

Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..

Vitu vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.
Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam Reviewed by WANGOFIRA on 13:47:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.