MPYA: TCU YATANGAZA SECOND ROUND APPLICATION KWA FORM SIX,DIPLOMA NA RPL 2016/2017

Image result for TCU.GO.TZ 
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)








TAARIFA KWA UMMA


Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.

       Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza

       Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza

       Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,

       Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,

       Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,

       Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.

Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.

Asanteni

Imetolewa na Prof. Eleuther Mwageni Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania 02 Septemba 2016


kwa maelezo zaidi bofya hapa
MPYA: TCU YATANGAZA SECOND ROUND APPLICATION KWA FORM SIX,DIPLOMA NA RPL 2016/2017 MPYA: TCU YATANGAZA SECOND ROUND APPLICATION KWA FORM SIX,DIPLOMA NA RPL 2016/2017 Reviewed by WANGOFIRA on 20:57:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.